• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 7:50 AM
Daraja la juu ya Thika Superhighway kujengwa Juja

Daraja la juu ya Thika Superhighway kujengwa Juja

NA LAWRENCE ONGARO

DARAJA la kivukio juu ya barabara kuu ya Thika Superhighway eneo la Highpoint, Gachororo, litajengwa ili kuzuia ajali za barabarani za kila mara.

Kwa muda mrefu wakazi wa eneo hilo wametoa malamishi wakidai kuwa karibu kila wiki wapitanjia hugongwa na magari yanayoendeshwa kwa kasi. Angalau watu 10 wamepoteza maisha yao kwa chini ya miezi mitatu.

Wahandisi wa Halmashauri ya Barabara Kuu Nchini (KeNHA) na Gavana wa Kiambu Dkt James Nyoro, walizuru eneo hilo mnamo Jumanne, na kuelezea mahali halisi litakapojengwa daraja hilo.

Gavana wa Kiambu Dkt James Nyoro (mwenye kofia nyeupe) akiwa na wahandisi wa KeNHA katika eneo la Highpoint, Juja mnamo Jumanne. PICHA | LAWRENCE ONGARO

Bw Anthony Mutua ambaye ni Mhandisi wa KeNHA alisema ujenzi wa daraja litakalogharimu Sh389 utazinduliwa haraka iwezekanavyo lakini kwenye barabara hiyo wataweka matuta ili kuzuia magari yanayoendeshwa kwa kasi kupunguza mwendo.

“Tunataka kazi hiyo ianzishwe mara moja. Hatutangoja chochote bali tutaanza kazi hiyo mara moja,” alifafanua mhandisi huyo.

Gavana Nyoro alisema Rais Uhuru Kenyatta aliingilia kati jambo hilo kiasi kwamba KeNHA imeahidi kuanza mradi huo baada katika muda wa wiki moja ijayo.

“Tungetaka kuona mpango huo ukitekelezwa haraka iwezekanavyo ili wakazi wa Juja na vitongoji vyake waweze kuishi bila wasiwasi amani,” alisema Dkt Nyoro.

Wakati wa ziara hiyo alikuwepo pia mhandisi wa KeNHA Francis Gitau aliyesema mradi huo utaharakishwa haraka iwezekanavyo ili kuzuia ajali zinazoshuhudiwa kila mara katika eneo hilo.

Alisema watafanya juhudi kutumia siku chache kabisa kukamilisha mradi huo.

Hivi majuzi Bw Aloise Kinyanjui ambaye ni mwaniaji wa kiti cha ubunge eneo la Juja aliongoza maandamano ya kulaani jinsi ajali nyingi za barabarani zinavyoendelea kushuhudiwa pahala hapo.

Bw James Nzuki ambaye ni mkazi wa kijiji cha Gachororo alisema ujenzi wa daraja hilo ukikamilika, watoto wa shule watanufaika pakubwa wanapovuka barabara hiyo ya Thika Superhighway.

  • Tags

You can share this post!

Munya ahimiza wakulima wakumbatie teknolojia za kisasa

KINYUA BIN KING’ORI: Polisi wasiegemee mrengo wowote...

T L