• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
Jamii yaiomba korti izuie operesheni za serikali Laikipia

Jamii yaiomba korti izuie operesheni za serikali Laikipia

Na RICHARD MUNGUTI

BARAZA la Jamii ya Maasai, Alhamisi waliwasilisha kesi mahakama kuu wakiomba operesheni ya maafisa wa usalama katika Kaunti ya Laikipia ikomeshwe mara moja.

Kwenye kesi hiyo iliyowasilishwa katika mahakama kuu na baraza hilo kupitia kwa mawakili Thomas Letangule na Abdi Noor, wafugaji wamepoteza zaidi ya ng’ombe 1,600 walio na thamani ya zaidi ya Sh160 milioni.

Mahakama imeelezwa wafugaji wameuawa na wengine zaidi ya 10 kujeruhiwa.Baraza hilo la wazee limeeleza shule zimefungwa na watoto wanaohofia maisha yao wako nyumbani.

Mahakama kuu iliambiwa wafugaji wasio na hatia wameathiriwa pakubwa kufuatia operesheni hiyo.

Wakiongozwa na wabunge wawili wa zamani David ole Sankori (Kajiado ya kati) na Peter Stephen Lenges pamoja na mwenyekiti wa baraza hilo Bw Kelena ole Nchoe wafugaji hao wanaomba korti isitishe operesheni hiyo inayoendelezwa na maafisa wa polisi.

Mabw ole Lenges, ole Nchoe na mwenyekiti wa baraza la wazee la Maasai, Kaunti ya Kajiado David ole Sankori wameeleza mahakama kuu haki za wafugaji zimekandamizwa na ng’ombe wao wamechukuliwa na maafisa wa usalama pasi na sababu.

Bw Letangule amesema wafugaji wamefujwa mali zao na sasa wanasukumiwa hali ya uchochole badala ya serikali kuwasaidia kujistawisha.

  • Tags

You can share this post!

Corona yaponda miji na vijiji

WASONGA: Serikali ikubali wazo la ODM uchumi ufunguliwe