• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 2:31 PM
Kachero wa DCI alijiua miezi miwili kabla ya kustaafu

Kachero wa DCI alijiua miezi miwili kabla ya kustaafu

NA BENSON MATHEKA

AFISA wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) aliyefariki baada ya kujipiga risasi Jumatano, alikuwa amebakisha miezi miwili astaafu.

Koplo Linus Mutunga, alikuwa na umri wa miaka  59 alipojipiga risasi ndani ya makao makuu ya DCI katika barabara ya Kiambu, Nairobi.

Kulingana na ripoti, afisa huyo alikuwa dereva katika idara hiyo na alikuwa astaafu mwishoni mwa mwaka huu wa 2023.

Ilisemekana kuwa afisa huyo aliondoka ofisini na kuelekea katika egesho la magari akionekana kuwa mtulivu. Ripoti zilisema alijifungia ndani ya gari kabla ya kujipiga risasi kichwani.

Mwili wake ulipatikana ndani ya gari kufuatia kisa hicho cha kujitoa uhai.

Polisi hawakupata ujumbe wowote alioandika kueleza sababu za kujitoa uhai na hakuwa amesimulia yeyote kuhusu masaibu yaliyomfanya kujiua.

Maafisa wa upelelezi wameanza kufanya uchunguzi kubaini kilichomfanya ajitoe uhai huku visa vya maafisa wa usalama kujitoa uhai vikiongezeka.

Tume ya Huduma ya Polisi imeimarisha mpango wa maafisa wa usalama kupata ushauri nasaha kufuatia visa hivyo vinavyohusishwa na mazingira ya kazi yao.

  • Tags

You can share this post!

Mlima Kenya unapigwa kiboko cha kisasi chini ya maji?

Wanafunzi wanane wanaoshukiwa kuteketeza bweni kuzuiliwa...

T L