• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 9:50 AM
Kaunti zalia kucheleweshewa mgao wa fedha za hazina ya kitaifa

Kaunti zalia kucheleweshewa mgao wa fedha za hazina ya kitaifa

Na SAMMY WAWERU

KAUNTI zimeonya kuwa huenda zikasitisha utoaji wa huduma zake hivi karibuni kufuatia kuendelea kucheleweshwa kwa mgao wa fedha za hazina ya kitaifa.

Serikali za ugatuzi zinasema zilipaswa kupata pesa kufikia mwishoni mwa juma lililopita.  Gavana wa Kiambu, Bw James Nyoro amesema ugumu wa utendakazi katika kaunti ukiendelea kushuhudiwa, hazitakuwa na budi ila kusimamisha utoaji wa huduma.

“Wizara ya Fedha na Hazina ya Kitaifa ilipaswa kutupa mgao kufikia Ijumaa iliyopita. Hadi kufikia sasa, hatujapata chochote,” Bw Nyoro akasema kwenye mahojiano ya kipkee na Taifa Leo.“Tunaendelea kusubiri kama Baraza la Magavana (CoG), huku tukifanya mazungumzo.

Kuanzia Juni 24, huenda tukasitisha utoaji wa baadhi ya huduma,” akaonya gavana huyo.Malalamishi ya serikali za kaunti kuhusu kucheleweshewa mgao, yanajiri majuma kadha baada ya Waziri wa Fedha Bw Ukur Yattani kusoma Makadirio ya Bajeti Mwaka wa Fedha 2021/2022.

“Tunaomba Wizara ya Fedha izingatie himizo letu. Si lazima tufunge kaunti, kwa sababu hatua hiyo itakuwa kunyima wananchi huduma wanazopasa kupata.Tayari baadhi ya kaunti zinaendeleza mgomo kwa sababu ya mishahara ya wafanyakazi kucheleweshwa,” Bw Nyoro akasema.

Gavana huyo hata hivyo alisema Kiambu imeweza kulipa wafanyakazi wake mshahara wa hadi Mei 2021.Alisema mwishoni mwa wiki hii, CoG itatoa taarifa kuhusu suala la kusitisha baadhi ya huduma.

Picha/ Sammy Waweru.
Gavana wa Kiambu, Bw James Njoro, pamoja na wenzake wanalalamikia Wizara ya Fedha na Hazina ya Kitaifa kucheleweshea serikali za kaunti mgao.

  • Tags

You can share this post!

Barabara kadhaa kufungwa kwa wakati tofauti

Maeneo bunge hayataongezewa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022,...