• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 3:36 PM
Maeneo bunge hayataongezewa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022, yasema IEBC

Maeneo bunge hayataongezewa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022, yasema IEBC

Na CHARLES WASONGA

MWENYEKITI wa Tume Huru ya Uchaguzi Wafula Chebukati Jumatano aliwaambia maseneta kwamba tume hiyo haitaweza kuongeza idadi ya maeneo bunge kabla uchaguzi mkuu ujao.

Akiongea alipofika mbele ya Kamati ya Seneti kuhusu Haki na Masuala ya Kisheria (SJLAC) Bw Chebukati alisema kulingana na mipango yake tume hiyo ina hadi mwaka wa 2024 kukamilisha shughuli hiyo.

“Haitutaweza kubadilisha mipaka ya maeneo bunge kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao. Hata yale maeneo bunge 70 yaliyopendekezwa katika mswada wa BBI hayataweza kubuniwa kabla ya uchaguzi huo ambao utafanyika Agosti 9, 2022,” Bw Wafula akaambia kamati hiyo inayoongozwa na Seneta wa Nyamira Okong’o Omogeni.

Bw Chebukati alifika mbele ya kamati hiyo kwa ajili ya kuifahamisha kuhusu maandalizi ya IEBC kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.Mwenyekiti huyo alisema tayari tume hiyo imeatangaza zabuni ya ununuzi wa vifaa vya kieletroniki vya kuendeshea uchaguzi maarufu kama (KIEMS Kits).

“Tulitangaza zabuni hiyo mapema ili kuzuia uwezekano wa kuharakishwa kwa ununuzi wa vifaa hivyo hali itakayochangia kununuliwa kwa vifaa vyenye dosari, ilivyofanyika katika chaguzi zilizopita,” Bw Chebukati akasema.

Kulingana na kipengeleza cha 89 cha Katiba, IEBC inahitajika kubadilisha mipaka ya maeneo wakilishi katika muda usiopungua mipaka minane au kuzidi miaka 12.

  • Tags

You can share this post!

Kaunti zalia kucheleweshewa mgao wa fedha za hazina ya...

Wakenya 36 kuwakilisha taifa Riadha za Dunia za Viziwi...