• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 11:48 AM
KDF ashtakiwa kwa kutafuna hongo ya Sh480,000

KDF ashtakiwa kwa kutafuna hongo ya Sh480,000

Na WAWERU WAIRIMU

AFISA wa Kikosi cha Ulinzi Kenya (KDF) ameshtakiwa kwa madai ya kupokea Sh480,000 kutoka kwa makurutu akiwahadaa kuwa watasajiliwa katika jeshi.

Haya yalielezwa Mahakama ya Jeshi wakati wa kikao cha kusikizwa kwa kesi hiyo jana katika Handaki ya Isiolo, Kikosi 78, iliyoongozwa na Hakimu Mkuu Isiolo Samuel Mungai.

Mwanajeshi huyo alishtakiwa dhidi ya kutekeleza hatia hiyo kuambatana na Kifungu 133 (1) b cha Sheria ya KDF 2012 (kupata pesa kwa njia ya udanganyifu kinyume na kipengele 313 cha Katiba).

Mwanajeshi huyo aliyewakilishwa na Wakili Manasses John Obetto, anashutumiwa vilevile dhidi ya kumtapeli Bw Nelson Kabwere Sh180, 000 katika eneo la Eastleigh, Nairobi, akiahidi pia kumsaidia kusajiliwa kama mwanajeshi,

Njama hizo za njia ya mkato zilitendeka siku chache tu kabla ya siku ya kusajili makurutu mnamo Disemba 6, 2019.

Hata hivyo, haijabainika wazi ni lini mshukiwa alikamatwa lakini vikao vya kusikizwa kwa kesi hiyo vilianza miezi miwili iliyopita kulingana na upande wa mashtaka.

Mashahidi saba tayari wametoa ushahidi kuhusu suala hilo.

  • Tags

You can share this post!

Uangalizi mdogo, mahitaji machache msukumo tosha wa kukuza...

Kaunti ya Nairobi pia yapitisha BBI