• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Kesi ya ubakaji dhidi ya mbunge kusikizwa hadharani

Kesi ya ubakaji dhidi ya mbunge kusikizwa hadharani

Na RICHARD MUNGUTI

ALIYEKUWA Mbunge wa Imenti ya kati Gideon Mwiti aliyeshtakiwa kwa ubakaji miaka sita iliyopita anataka kesi hiyo isikizwe adharani.

Wakili Dkt John Khaminwa anayemwakilisha Mwiti alimweleza hakimu mkuu anataka kesi inayomkabili mteja wake isikizwe adharani na wala sio kwa njia ya mitandao.

“Kutokana na umuhimu wa kesi hii naomba hii mahakama isikize kesi hii adharani badala ya mshtakiwa kuombwa afungue kompyuta kusikiza kesi,” alisema Dkt Khaminwa

Kiongozi wa mashtaka Bi Angela Fuchaka alieleza mahakama hapingi ombi hilo ila itategemea jinsi hali ya ugonjwa wa corona itakavyokuwa nchini.

Hakimu aliamuru kesi hiyo itajwe Juni 16,2021 kwa maagizo zaidi.

Mwiti amekanusha mashtaka matatu ya kubaka, kutisha na kumwuumiza malalamishi.

Mwanasiasa huyo ameshtakiwa pamoja na Dkt David Muchiri anayedaiwa alikuwa anawapima wanawake iwapo wako na ukimwi kabla ya kuonana na mwanasiasa.

Majaribio ya awali ya Bw Mwiti ya kutamatisha kesi hiyo ilikataliwa na Jaji Weldon Korir na pia Bw Andayi aliyesema mashtaka dhidi ya washtakiwa yameorodheshwa kwa mujibu wa sheria.

  • Tags

You can share this post!

CECIL ODONGO: Mbinu anazoweza kutumia Ruto ili kutwaa urais...

TANZIA: Mhariri wa zamani wa Taifa Leo afariki