• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 8:50 AM
Kusema ‘hatupangwingwi’ si uchochezi – mahakama

Kusema ‘hatupangwingwi’ si uchochezi – mahakama

NA RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA Kuu ilifutilia mbali sheria ya kupiga marufuku na kuharamisha maneno “hatupangwingwi” na “watajua hawajui”.

Maneno hayo yalikuwa yameharamishwa na Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC).

NCIC ilharamisha matumizi ya maneno hayo mnamo Aprili 8, 2022.

Akifutilia mbali sheria hiyo Jaji Ant0ny K Ndung’u alisema “maneno hayo si ya uchochezi.’’

Jaji Ndung’u alikubali ombi la vuguvugu la Chama cha Mawakili Limited (CML) kupitia mawakili Felix Kiprono na Vincent Yegon kufutilia mbali sheria hiyo.

Kiprono aliomba korti itupilie mbali sheria hiyo akisema serikali itaanza kuwakamata wanasiasa na kuwafungulia mashtaka kwa kutumia maneno hayo.

Jaji huyo alisema hakuna mtu aliyechochewa na maneno hayo.

  • Tags

You can share this post!

Sonko anahatarisha kura Mombasa – IEBC

UFUGAJI: Jinsi anavyojipatia riziki kwa kuwafuga sungura

T L