• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 5:50 AM
Mahakama yaharamisha bomoabomoa za kiholela

Mahakama yaharamisha bomoabomoa za kiholela

NA PHILIP MUYANGA

MAHAKAMA imeamua kuwa ubomoaji wa majengo kiholela wakati wa mizozo ya umiliki wa ardhi ni hatia.

Katika uamuzi ambapo Mahakama ya Mazingira na Ardhi iliamuru Serikali ya Kaunti ya Kilifi kumlipa mmiliki wa ardhi fidia ya Sh4 milioni, Jaji Sila Munyao alisema ubomoaji unaweza tu kufanywa kama njia ya mwisho kabisa.
Mahakama ilisema hatua hiyo inaweza kuchukuliwa tu pale ambapo licha ya mjenzi kupewa nafasi na wakati wa kujirekebisha, ni tishio kwa mazingira au kukiuka haki za wengine.

Kaunti ilipatwa na hatia ya kubomoa ukuta wa Bw Farid Faraj, kwenye eneo la ufuo wa Mtwapa.
Jaji Munyao pia aliamuru serikali ya kaunti kumlipa Bw Faraj Sh1 milioni kama fidia ya jumla kwa uvunjaji sheria alisema kuwa kitengo cha ugatuzi kiliharakisha na kubomoa ukuta huo bila kumpa fursa ya kujitetea.

  • Tags

You can share this post!

Ashtakiwa kwa kutaka kumuua dadake Raila

Ramadhan: Serikali yaondoa ushuru kwa uagizaji wa tende

T L