• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 11:53 AM
Mbote asema wanafunzi walimpa changamoto

Mbote asema wanafunzi walimpa changamoto

Na RICHARD MUNGUTI

MCHAKATO wa kumtafuta atakayemridhi David Maraga kuwa Jaji Mkuu uliingia siku yake ya pili huku msomi mtajika na mwenye tajriba ya juu katika somo la uanasheria Prof Kameri Mbote Annie Patricia Gathiru akisema changamoto kuu aliyowahi kumbana nayo ni wakati wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi (UoN) waliweka baa na kucheza muziki wa Ndobolo ya Solo.

Alisema wanafunzi walikuwa wakicheza ‘Ndobolo’ nje ya afisi yake na kulewa chakari. Pia alisema akiwa naibu wa mkuu wa UoN wahuni walivamia uchaguzi wa wawakilishi wa wanafunzi katika seneti na kuuvuruga huku baadhi ya wanafunzi wakisalia miezi miwili kuhitimu.

Alisema ilibidi wanafunzi hao watimuliwe chuoni lakini “baadaye akajihoji na kuomba waruhusiwe kuendelea na masomo.”

Msomi huyo alisema kuwa alikabiliwa na kipindi kigumu wakati alinyimwa fursa ya kuongoza kitivo cha sheria.

“Baada ya kusomesha sheria kwa miaka zaidi ya sita nilinyimwa fursa ya kuongoza kitivo hicho. Nilichukua likizo ya miaka mitatu nikaanzisha kitivo cha sheria chuo kikuu cha Strathmore kukipa chuo kikuu cha Nairobi ushindani,”alikumbuka.

Lakini akiwa mle utafiti aliofanya kuhusu umiliki wa mali ukaibwa na wanafunzi wake watatu wakachapisha kitabu kinachotumika hata waleo.

Kwa sababu ya uvumilifu na subiria aliwasamehe. “Nilitaka kuanzisha shule ya kutoa mafunzo ya uanasheria lakini nikaamua kurudi kusomesha UoN hadi wa leo,” alisema Prof Mbote.

Alisema changamoto alizopata akiwa mhadhiri zimechangia kumuunda kuwa na weledi wa hali ya juu katika usimamizi wa asasi mbali mbali.

Alieleza JSC kuwa amehitimu katika kozi chungu nzima ambazo zimemwezesha kutangamana na wasomi wakuu ulimwenguni.

“Nimewafundisha wasomi wa sheria zaidi ya 6,000 ulimwenguni na hao watasaidia katika kuboresha uhusiano wa idara ya mahakama.

Prof Mbote alifika mbele ya tume ya kuajiri watumishi katika idara ya mahakama (JSC) inayoongozwa na aliyekuwa VC wa Chuo kikuu cha Kenyatta (KU) Prof Olive Mugendi kuhojiwa.

Akijieleza mbele ya JSC Prof Kameri Mbote Annie Patricia Gathiru alisema kazi ya Jaji Mkuu inahitaji mtu msikifu, mvumilivu na mwenye subira ya hali ya juu.

Prof Mbote alijipigia debe akisema yuko na ufahamu unaotosha kuongoza idara ya mahakama.

Alisema amekuwa mkuu wa asasi mbali mbali katika mataifa zaidi ya 60 barani Afrika kuhusu suala la sheria na “anaamini ataweza kumridhi Bw David Maraga kuwa Jaji Mkuu wa tatu tangu katiba ya 2010 ipitishwe.”

Akihojiwa na makamishna wa tume ya kuajiri watumishi wa idara ya mahakama JSC , Prof Mbote alisema yuko na uwezo wa kuongoza idara ya mahakama iliyo na wafanyakazi zaidi ya 5,000.

Kuhusu mbinu za kufanikisha uhusiano kati ya idara ya mahakama ya Kenya. Alisema usawa wa kijinsia unahitajika.

Akijibu maswali ya kamishna Macharia Njeru aliyeungama yuko na mzazi mmoja alisema jamii imekuwa ikiwadhulumu kina mama.

Hata Prof Mbote alisema kunwa nyakati amekuwa akisimangwa na wasomi wanaume kutokana na kimo chake.

Alisema mahakama zinapasa kutoa maamuzi kulingana na sheria asili kutokana miundo msingi ya kijamii.

  • Tags

You can share this post!

Wageni waliopata chanjo ya corona China wasema ni salama

Bei ya mafuta haitabadilika – Serikali