• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 5:50 AM
Mchungaji adaiwa kupotosha waumini kuwanyima watoto chakula ‘wakaurithi ufalme wa mbinguni’

Mchungaji adaiwa kupotosha waumini kuwanyima watoto chakula ‘wakaurithi ufalme wa mbinguni’

NA ALEX KALAMA 

MAAFISA wa Idara ya Kuchunguza Makosa ya Jinai (DCI) mjini Malindi katika Kaunti ya Kilifi wamemtia mbaroni mchungaji Paul Makenzi wa kanisa la Good News International ambaye anadaiwa kuwapotosha wakazi wa eneo la Shakahola, kwa kuwataka kutowapa watoto wao chakula jambo ambalo limechangia idadi kubwa ya watoto kuaga dunia.

Kulingana na baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakiongozwa na Francis Wanje, ambaye anadai kuwa tayari wajukuu wake wawili waliaga dunia baada ya wazazi wao kupata mafunzo kutoka kwa mchungaji huyo, ambaye aliwashurutisha watoto hao kuingia katika mfungo hadi pale ambapo wangedhoofika na kufariki.

Akizungumza na wanahabari wakati wa operesheni ya kukamata mchungaji huyo, amesema kuwa mchungaji huyo amekuwa akidai kuwa yapo majanga ambayo huenda yakashuhudiwa katika siku za usoni na hivyo basi ni vyema kwa watoto hao kuaga dunia ili waurithi ufalme wa mbinguni.

“Wajukuu wangu wawili tayari wameshazikwa alikuwa na yule mmoja ambaye amekuwa amebaki na tayari alikuwa anamtayarisha afariki na apate kupumzika. Mchungaji wao aliwambia kuna majanga ambayo yanakuja karibuni si vizuri majanga haya yaweze kuwapata na akaagiza sasa wasipatiwe chakula mpaka wafe, wajukuu wangu walikufa katika hali hiyo na sasa hii tumefika na maafisa wa ujasusi tukienda kwa mchungaji ili wakamkamate,” alisema Bw Wanje.

Vile vile ameibua madai ya takriban watoto 30 kuzikwa baada ya kuaga dunia katika hali hiyo, jambo ambalo bado maafisa wa polisi hawajathibitisha.

“Kufikia sasa inasemekana ya kwamba zaidi ya watoto 30 tayari wameshazikwa na wanasema kwamba watoto wote wakiisha itakuwa sasa ni zamu ya kina mama nao wafe wote wamalizike kabla ya hili janga kutokea. Achukuliwe hatua kali sana amepoteza maisha ya watoto wachanga ambao hatachawana hatia serikali tafadhali iweze kuchukua hatua mahususi hasa katika madhehebu ambayo hayaeleweki,” alisema Bw Wanje.

Aidha kamanda wa polisi eneo la Malindi John Kemboi amethibitisha kukamtwa kwa mchungaji huyo na kuahidi kutoa taarifa kamili kuhusu idadi ya watoto walioaga dunia na taarifa nyingine nyingi kuhusiana na tukio hilo hapo kesho Jumatano.

  • Tags

You can share this post!

Kaunti ya Vihiga yasaka ‘Fuliza’ kutoka kwenye benki

Simbas kucheza dhidi ya Namibia, timu nyingine nane Currie...

T L