• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 2:31 PM
Mwanamuziki maarufu Muhiko Nebster aaga dunia

Mwanamuziki maarufu Muhiko Nebster aaga dunia

NA WANDERI KAMAU

MWANAMUZIKI maarufu wa nyimbo za injili kwa lugha ya Kikikuyu kutoka eneo la Kati, Muhiko Nebster, ameaga dunia.

Mmoja wa wanafamilia yake amesema kuwa mwanamuziki huyo alifariki usiku wa kuamkia leo Jumatano, Oktoba 18, 2023.

“Marehemu amekuwa akiugua kwa muda. Tutatoa maelezo zaidi,” amesema jamaa mmoja kwenye mahojiano na Taifa Leo.

Alikuwa miongoni mwa wanamuziki ambao walikuwa wakisifiwa kwa kuimba nyimbo za kuwatetea raia kutokana na changamoto tofauti ambazo wamekuwa wakipitia, kwa mfano, dhuluma za kisiasa na kiuchumi kutoka kwa tawala zilizopo.

Alizaliwa katika eneo la Kangema, Kaunti ya Murang’a. Baadaye, mamake alihamia katika eneo la Banana, Kaunti ya Kiambu, alipokuwa na umri wa miaka saba.

Amekuwa katika ulingo wa muziki kwa zaidi ya miaka 20 na baadhi ya nyimbo zake zilizosifika sana ni ‘Mwari wa Milionea’ (Bintiye Tajiri), ‘Tuhe Mbia Baba’ (Tujaalie Pesa Baba) alioshirikiana na mwanamuziki Muigai wa Njoroge, ‘Tinii Wonire’ (Si Mimi Uliyeona) kati ya nyingine nyingi.

Mashabiki wake kwenye mitandao ya kijamii wamemuomboleza kama “mwanamuziki aliyetumia kipaji chake kuwatetea wanyonge.”

“Nimeshtuliwa sana na kifo chake cha ghafla. Mungu ailaze roho yake pahala pema peponi,” amesema Bw James Mwaniki.

  • Tags

You can share this post!

Linturi akemea Nacada akisema miraa, muguka si dawa za...

Fahamu namna ya kukwepa mtego wa matapeli wa uuzaji na...

T L