• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 6:50 AM
Mwanawe waziri wa zamani aponyoka kitanzi

Mwanawe waziri wa zamani aponyoka kitanzi

Na RICHARD MUNGUTI

MWANAWE wa kambo wa waziri msaidizi wa zamani Betty Tett ambaye alikuwa amehukumiwa kunyongwa kwa kumnyang’anya babake mlezi pesa kimabavu jana aliponyoka kitanzi hukumu hiyo ilipobatilishwa.

Hakimu mkuu Francis Andayi alibatilisha adhabu ya kunyongwa dhidi ya David Tett na kifungo cha miaka 15.

Bw Andayi alitoa adhabu hiyo kufuatia agizo la Jaji James Wakiaga, kuamuru mfungwa huyo ahukumiwe tena. David alihukumiwa na aliyekuwa hakimu mkuu Kiarie Waweru alipompata na hatia ya wizi wa mabavu.

Hakimu huyo wa zamani aliyeteuliwa kuwa Jaji mahakama kuu alisema upande wa mashtaka ulithibitisha David alikuwa miongoni mwa majambazi waliovamia makazi ya William Tett mtaa wa Karen na kumnyangánya pesa, kadi za benki na bidhaa vya thamani ya Sh157,000.

David alikata rufaa akipinga adhabu hiyo akisema haikuzingatia haki zake.Jaji Wakiaga alikataa kufutilia mbali adhabu ya kunyongwa iliyopitishwa na Jaji Kiarie.

Jaji Wakiaga aliamuru mshtakiwa ahukumiwe upya.Kufuatia agizo hilo, Bw Andayi alimuhukumu David atumikie kifungo cha miaka 15 kuanzia siku ile alishikwa na kuzuiliwa mnamo 2011.

David aliyelamaa akiwa gerezani aliondolewa kwa kiti cha magurudumu kutoka mahakamani kuanza kutumikia kifungo kipya.

Aliposhtakiwa mbele ya Jaji Kiarie 2014, David alieleza korti kesi aliyoshtakiwa inatokana na uhasama wa kifamilia.

Lakini upande wa mashtaka ulipinga madai hayo na kuwasilisha ushahidi kwamba mshtakiwa aliongoza genge la majambazi kumpora baba yake wa kambo.

You can share this post!

Munya atangaza kupigania ugavana Meru

DCI yachunguza kisa cha watoto kufungwa