• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Ndugu wawili wakana kuibia Benki ya Dubai Sh154milioni

Ndugu wawili wakana kuibia Benki ya Dubai Sh154milioni

Na RICHARD MUNGUTI

NDUGU wawili Jumatano walishtakiwa kuibia benki iliyofilisika ya Dubai (DBK) Sh154milioni miaka 14 iliyopita.

Bw Kirpal Singh aliye na umri wa miaka 78 na Amarjeet Singh, 72 walifikishwa mbele ya hakimu mkuu mahakama ya Milimani Francis Andayi.Na punde waliposomewa mashtaka wakili Robert Githui anayewatetea alieleza hakimu washtakiwa waliondolewa lawama katika kesi ya mahakama kuu.

“Ndugu hawa hawana hatia. Waliondolewa lawama na wasimamizi wa benki hii,” Bw Githui alieleza hakimu.Wawili hao walikanusha mashtaka manne dhidi yao na kuomba waachiliwe kwa dhamana.Kirpal na Amarjeet walidaiwa waliiba pesa hizo kupitia akaunti za kampuni yao Kamp General Engineers Company.

Mahakama ilielezwa pesa zilikuwa zapitishwa kwenye akaunti ya kampuni hii ambayo washtakiwa ni wakurugenzi.Kiongozi wa mashtaka Bi Angela Fuchaka hakupinga washtakiwa wakiachiliwa kwa dhamana.

Kila mmoja aliachiliwa kwa dhamana ya Sh1milioni pesa tasilimu.Kesi hiyo itaunganishwa na nyingine ambapo mmiliki wa benki hiyo iliyowekwa chini ya mrasimu wa benki kuu ya Kenya Hassan Mohamed Zubeid ameshtakiwa.

Bi Fuchaka alisema kesi hiyo dhidi ya Zubeid itasikizwa Agosti 9, 2021.Washtakiwa hao walikana waliiba pesa hizo kati ya 2007 na 2019..

  • Tags

You can share this post!

Ruto akatwa mbawa

Nilipokuwa Naibu Rais kazi bora ilifanyika – Ruto