• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
Polisi sita wapinga kushtakiwa kwa mauaji

Polisi sita wapinga kushtakiwa kwa mauaji

Na RICHARD MUNGUTI

MAAFISA sita wa polisi wanaozuiliwa kufutia vifo vya ndugu wawili kaunti ya Embu wanaomba Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) azimwe kuwafungulia mashtaka ya mauaji.

Polisi hao pia wanaomba mahakama kuu iamuru miili ya wavulana hao ifukuliwe ifanyiwe upasuaji kama “wamewakilishwa na mawakili na daktari wao.”Sita hao wanasema ripoti ya Dkt Johansen Oduor ilionyesha ndugu hao walikufa kutokana na kichapo kwa kifaa butu.

“Washukiwa hao hawakuwakilishwa na wakili au daktari wao katika zoezi hilo la upasuaji wa miili ya ndugu hao ili kukubaliana na uamuzi uliofikiwa,” Bw Omari alisema.Sita hao wanadai vijana hao waliruka kutoka kwa gari la polisi walipokuwa wanapelekwa katika kituo cha polisi cha Manyatta wakiwa na mahabusu wengine wanane.

Washukiwa hao wanaomba mahakama iamuru uchunguzi ufanywe kubaini kilichosababisha vifo vya wavulana hao.“Polisi wanaozuiliwa hawakuwaua wavulana hao kamwe mbali waliruka gari ya polisi ikienda kasi na kufyata lami kisha wakakata roho,” asema wakili Danstan Omari.

Bw Omari aliambia Taifa Leo ushahidi uliorekodiwa na mahabusu walioshikwa pamoja na wahasiriwa hao wawili ni kwamba “waliwaona wakijirusha kutoka kwenye gari la polisi huku wakidhani wameponyoka na kukwepa kufikishwa kortini.”

Polisi wanaozuiliwa ni Koplo Benson Mbuthia, Koplo Consolata Kariuki , Nicholas Sang Cheruiyot, Martin Msamali Wanyama , Lilian Cherono Chemuna na James Mwaniki.Pia mahakama inaombwa iamuru washukiwa hao warudishiwe simu zao wawasiliane na benki zao watoe pesa za kuwalipia karo watoto wao.

Washukiwa hao wanasema hawana pesa za kukimu mahitaji ya familia zao na pia ada ya mawakili kwa vile hawawezi toa pesa kwa akaunti kwa vile “simu zilichukuliwa na polisi.”Washukiwa hao wanachunguzwa kwa lengo la kuwashtaki kwa mauaji ya Benson Njiru Ndwiga, 22na Emmanuel Mutura Ndwiga, 19

Bw Omari amesema kinyume cha vile  ilidaiwa kuwa polisi waliteketeza gari iliyokuwa imewabeba vijana hao , ni wananchi waliokuwa na hasira walioiteketeza wakati wa kukabiliana na waandamanaji.Wakili huyo alisema kuwa baada ya wavulana hao kujirusha polisi wa idara ya trafik ndio walichunguza kesi hiyo na hata kuipeleka  kukaguliwa kisha ikarudishwa katika kituo cha polisi kufanya kazi nyingine.

“Ushahidi uliopo ni kuwa vijana hao hawakuuliwa msituni na maiti zao kupepelekwa Mochari.Walijiua kwa kujirusha kutoka kwa gari la polisi,” alisema Bw Omari.Polisi hao wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Capital Hill hadi Agosti 30 watakapofikishwa kortini kujibu mashtaka ya mauaji.

  • Tags

You can share this post!

Ukatili wa Jungle FC kwa wapinzani waizolea sifa tele mjini...

Pendekezo wabunge wapitishe ‘matunda’...