• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 8:50 AM
Polisi wamsaka mmiliki wa lori lililosafirisha bangi

Polisi wamsaka mmiliki wa lori lililosafirisha bangi

NA JACOB WALTER

MAAFISA wa usalama wanamsaka mmiliki wa lori lililokamatwa likibeba magunia 64 ya bangi ya thamani ya Sh45 milioni katika lokesheni ya Sololo mnamo Ijumaa.

Kamishna wa Kaunti ya Marsabit Paul Rotich ameeleza kuwa uchunguzi unaendelea kumkamata mwenye gari hilo aina ya Mitsubishi Fuso lililokuwa likibeba shehena hiyo ya dawa za kulevya.

“Uchunguzi unaendelea, na tunafanya kila juhudi kumkamata mmiliki wa gari lililohusika,” akasema Bw Rotich.

Mkuu wa polisi wa Moyale (OCPD) Walter Kiptala, alisema kwamba wanaendelea na uchunguzi na hawawezi kufichua maelezo zaidi wasihatarishe juhudi zao.

Aliahidi kuelezea wanahabari punde tu baada ya uchunguzi kukamilika.

Polisi walianza uchunguzi huo baada ya kukamata bangi ya Sh45 milioni katika eneo la Dambalaf , Fachana, kaunti ndogo ya Moyale mnamo Ijumaa.

Akizungumza na Taifa Leo kwa simu kamanda wa polisi kaunti ya Marsabit Robinson Mboloi alisema kwamba lori hilo aina ya Mitsubishi Fuso nambari za usajili KCR 003A lilikamatwa kwenye barabara moja ndogo eneo hilo.

“Tunachukulia kisa cha hivi punde kama cha kawaida kwa kuwa umepita muda mrefu baada ya watu kadhaa kukamatwa mwaka jana kwenye barabara ya Moyale-Isiolo. Tuko chonjo kuhakikisha hakuna mihandarati inaingia katika nchi hii kupitia mpakani,” akasema Bw Mboloi.

  • Tags

You can share this post!

Mbunge aahidi kupigania akina mama bungeni

SHINA LA UHAI: Tatizo la kigugumizi linakumba zaidi watoto...

T L