• Nairobi
  • Last Updated May 16th, 2024 8:50 PM
Raila aapa kuandaa maandamano licha ya onyo la serikali

Raila aapa kuandaa maandamano licha ya onyo la serikali

NA SAMMY WAWERU

KINARA wa Azimio Raila Odinga ameshikilia kwamba maandamano yaliyopangwa kufanyika jijini Nairobi mnamo Jumatatu wiki ijayo, lazima yaendelee.

Bw Raila amesema ‘njia’ aliyochukua, inalenga kusaidia kukomboa nchi ya Kenya.

“Siwezi kutishwa na yeyote, tarehe 20 (akimaanisha Jumatatu, Machi 20) tutaonana na wao ana kwa ana,” akasisitiza.

Msimamo wa kiongozi huyo wa upinzani, umeonekana kukaidi amri ya serikali kuhusu maandamano yenye ghasia.

Baadhi ya maeneo nchini hasa ngome za upinzani, yameshiriki maandamano yaliyoshuhudia vurugu na uharibifu wa mali na baishara za watu.

Rais William Ruto amesema hata ingawa ni haki Kikatiba upinzani kushiriki maandano, ameonya serikali haitaruhusu vurugu kuzuka wala uharibifu wa mali.

Kulingana na Raila, maandamano anayoandaa ni ya amani. “Unaweza ukanizuia mimi mwenyewe, ila mawazo yangu hutayaweza,” akasema Waziri Mkuu huyo wa zamani, akihutubia umma Alhamisi katika Kaunti ya Nakuru.

Raila amekuwa akiandaa mikutano ya kisiasa sehemu tofauti nchini, na kutumia majukwaa hayo kupinga uhalisia wa serikali ya Kenya Kwanza.

  • Tags

You can share this post!

Omanga kuwa CAS Wizara ya Usalama wa Ndani akipitishwa na...

Omanga ‘amcheka’ Raila kwa kutishia kumshtaki Rais

T L