• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 11:59 AM
Shule za upili kuorodheshwa kwa uwezo wa CBC

Shule za upili kuorodheshwa kwa uwezo wa CBC

REGINAH KINOGU na GEORGE MUNENE

SHULE za upili za kiwango cha chini zitaorodheshwa kulingana na idadi ya vifaa zilivyo navyo kuwawezesha wanafunzi kuendelea na masomo ya Umilisi na Utendaji (CBC).

Kulingana na Waziri wa Elimu, Prof George Magoha, viwango vitatu ambavyo vitazingatiwa katika kuamua mwelekeo wa kitaaluma wa mwanafunzi ni sanaa na sayansi ya michezo, sayansi ya jamii na sayansi ya jamii, teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM).

Kwenye ziara katika Kaunti ya Nyeri jana Jumatano, Prof Magoha alisema shule zenye vifaa na miundomsingi bora zitafunza viwango vyote vitatu, huku zile zenye uwezo wa kadri zikifunza viwango viwili.

Shule zilizoorodheshwa kuwa za kiwango cha kadri ni za kutwa na baadhi ya zile za mabweni.

“Pengine hatutatumia utaratibu wa awali kama vile shule za kitaifa, kaunti au wilaya. Hata hivyo, ikiwa zitakuwa na uwezo wa kufunza masomo hayo yote, basi huenda zikaorodheshwa kwa mfumo huo,” akasema.

Hilo linamaanisha kuwa shule zote 103 za kitaifa na kiwango cha kaunti zitakuwa zikitoa mafunzo kwa viwango vyote vitatu vya masomo huku zile ndogo zikitoa mafunzo kwa viwango viwili pekee.

Wanafunzi wa Gredi ya Sita wanatarajiwa kujiunga na Shule ya Upili ya Kiwango cha Chini baada ya kumaliza mitihani yao.

Wanafunzi hao, ambao walisoma kwa miaka miwili katika kiwango cha chekechea, watasoma miaka sita katika shule ya msingi, miaka sita katika shule ya upili na miaka mitatu katika chuo kikuu na taasisi nyingine za masomo ya juu.

Wanafunzi walio katika Gredi za Nne na Tano watafanya mitihani yao ya kitaifa kati ya Januari 31 na Februari 4.

Hili ni baada ya kufanya mitihani tekelezi kati ya Oktoba na Desemba 2021.

Mitihani hiyo itachangia asilimia 20 ya alama zao za mwisho watakazopata kwenye mtihani wa Gredi ya Sita.

Mtihani wa mwisho utachangia asilimia 40 ya jumla ya alama zao.

Kuhusu ujenzi wa madarasa ya shule hizo za upili, waziri alisema ujenzi wa baadhi ya madarasa ushakamilika.

  • Tags

You can share this post!

KINYUA BIN KING’ORI: Wanasiasa sharti wachague kwa...

Vitushi katika Onyesho la Pili, Tendo la Pili la Tamthilia...

T L