• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 9:16 PM
Vitushi katika Onyesho la Pili, Tendo la Pili la Tamthilia – Kigogo

Vitushi katika Onyesho la Pili, Tendo la Pili la Tamthilia – Kigogo

JUMA lililopita tuliangalia onyesho la pili tendo la kwanza.

Leo tutatalii onyesho la pili, tendo la pili. Tendo hili linapoanza, Majoka amemshika mkewe – Husda mikono ili asimrukie Ashua. Husda anabwata.(uk 26)

Kwa mhemko anasema atamuua Ashua kwa sababu Majoka haonekani nyumbani – anamshuku kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na Ashua. Majoka anamwambia achunge ulimi wake. Husda anamwambia mumewe kuwa wa kujichunga ni yeye na hawara wake.

Ashua anamkanya asimwite hawara kwani Majoka amemtusi vya kutosha.

Majoka anamwachilia Husda mkono na kutishia kumchafua akileta fujo hapo ofisini, anasema wanawake ni wanawake tu (maudhui – udunishaji wa mwanamke).

Ashua na Husda wanajibizana kwa ukali na hasira. Majoka anadokeza kuwa alikuwa amemwita mkewe ofini (maudhui – ulaghai) Husda anamkabili Ashua kwa hasira, anamtusi kuwa yeye ni kidudumtu, stesheni ya udaku na mwenye kuwinda wanaume wa watu.

Majoka anajaribu kumtuliza Husda aache kumtusi Ashua. Husda anamrukia Ashua na kumwangusha. Majoka anasimama kando huku akimtazama Ashua akizabwa makofi. Sauti ya Kenga inasikika mawazoni mwa Majoka kuwa akubali pendekezo la kufungwa kwa soko kwani ni fursa nzuri ya kulipiza kisasi kwa huyo Sudi na kumnasa Ashua.

“Ashua akija ofisini mwako, mtumie mkeo ujumbe aje osifini, watakabiliana, amuru askari wamtie Ashua nguvuni kwa madai ya kuzua vurugu katika ofisi ya serikali,” (maudhui – ulaghai).

Majoka anawatenganisha Husda na Ashua kwa ukali. Anawaamuru Chopi (mlinzi wa Majoka) na Mwango (askari katika makazi ya Majoka) wawafungie Husda na Ashua ndani.

Ashua anamtafadhalisha Majoka asimfungie kwa sababu ananyonyesha huku wanawe wakilala njaa.Mwango na Chopi wanawatia Ashua na Husda ndani.

Agizo linatolewa kuwa Husda atolewe baada ya nusu saa. Kisha dereva wake aje ampeleke nyumbani na ampikie mumewe chapati kwa kuku (uk 30).

Simon Ngige

Alliance High School

You can share this post!

Shule za upili kuorodheshwa kwa uwezo wa CBC

Rais Kenyatta atoa wito kwa viongozi kushirikiana kwa...

T L