• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 5:50 AM
Uhuru asema waangalizi wako macho nchini Nigeria

Uhuru asema waangalizi wako macho nchini Nigeria

NA WINNIE ONYANDO

RAIS (Mstaafu) Uhuru Kenyatta ambaye anaongoza ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi Nigeria amehakikishia nchi hiyo uchaguzi wa amani.

Alikabidhiwa jukumu hilo na Umoja wa Afrika (AU) wiki chache zilizopita.

Hili ni jukumu la pili la kikanda analotekeleza Rais huyo tangu astaafu Septemba 2022.

Bw Kenyatta aliwasili katika nchi hiyo Februari 21, 2023.

Uchaguzi unatarajiwa kufanyika Jumamosi, Februari 25.

Akihutubia wanahabari muda mchache baada ya kukutana na wajumbe wengine, Bw Kenyatta alisema jukumu lake kuu ni kuhakikisha kwamba, uchaguzi unafanyika kwa amani.

“Tuko hapa kuhakikisha wananchi wote wanatekeleza jukumu lao la kumchagua kiongozi wanayempenda,” akasema Bw Kenyatta.

Kuna jumla ya wagombeaji 18 ila ni watatu pekee walio na nafasi ya kushinda kiti hicho, kulingana na kura za maoni. Nchi hiyo imekuwa ikikabiliwa na utovu wa usalama, kuzorota kwa uchumi, uhaba wa pesa, kupanda kwa gharama ya maisha na mashambulizi ya kiholela.

  • Tags

You can share this post!

Matamshi yenu yapaswa kuambatana na vitendo, Askofu Muheria...

Kenya yadaiwa deni la Sh639 bilioni na raia wake

T L