• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 5:55 AM
Ulevi wa wanafunzi Murang’a mjini wakera wenyeji 

Ulevi wa wanafunzi Murang’a mjini wakera wenyeji 

NA MWANGI MUIRURI 

WAKAZI wa Mji wa Murang’a wameelezea masikitiko yao na jinsi vitengo vya kiusalama huruhusu wanafunzi kuponda raha kwa kunywa pombe usiku kucha.

“Ikiwa kuna Kaunti ambayo ina maafisa ambao hawasaidii wazazi kudhibiti watoto wao wanaosomea katika taasisi za Murang’a, ni hii. Kuanzia jioni hadi asubuhi unapata tu wanafunzi hao wa kike na wanaume wakiyumbayumba wakiwa walevi,” akasema Bw Simon Mburu, mkazi.

Mji wa Murang’a huwa na wanafunzi wa taaluma ya uuguzi (KMTC) na pia chuo Kikuuu Cha Murang’a.

Bi Beatrice Kiilu alisema kwamba “bora tu maafisa wa kiusalama wamepata chai yao, hawajali wanafunzi kuuziwa ulevi usiku kucha na hata kucheza densi katika vilabu vya uchi vilivyoko katika mji huu”.

Bi Kiilu alisema kwamba “ni aibu kubwa kwa serikali kuwa shabiki wakati rasilimali za wazazi zinatumiwa kufadhili ulevi ikijulikana vyema mabaa hayo yanahujumu kesho ya watoto hao”.

Baadhi ya wanafunzi waliozungumza na Taifa Leo Dijitali walisema kwamba ulevi ni burudani na huwa wanautumia kupigana na uchovu wa masomo.

“Tukishikwa sisi hutoa tu Sh50 na polisi wanatuachilia tupige sherehe. Kuna mabaa ambayo ni yetu spesheli. Maafisa huwa hawatusumbui sana bora tu tusirandarande sana,” akasema Pius Kioko.

Visa vya wanafunzi huo kudhulumiwa kimapenzi wakiwa walevi chakari vimezidi mtaani humo, mmoja wao akiripotiwa kujitia kitanzi miezi miwili iliyopita baada ya kulewa usiku kucha.

 

[email protected]

 

  • Tags

You can share this post!

Mahakama yazima uhuru wa polisi wa kibajeti waliopewa na...

Ajabu mwanamke mjamzito ‘kujifungua’ akiwa chooni bila...

T L