• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 8:55 AM
Vita vya Uhuru na mahakama vingalipo

Vita vya Uhuru na mahakama vingalipo

Na SAMMY WAWERU

RAIS Uhuru Kenyatta ameendeleza mashambulizi yake kwa idara ya mahakama, kufuatia uamuzi wa korti kuharamisha Ripoti ya Mpango wa Maridhiano (BBI).

Mei, mahakama kuu iliharamisha mswada huo wa marekebisho ya Katiba 2020, ikiutaja kama “mpango haramu kukarabati Katiba na ambao haukufuata sheria”.

BBI iliasisiwa na Rais Kenyatta na kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, baada ya viongozi hao kutangaza kuzika tofauti zao za kisiasa mnamo Machi 2020, kupitia Handisheki.

Katika hafla ya maadhimisho ya Madaraka Dei 2021, Jumanne, Kisumu, Rais Kenyatta aliendeleza mashambulizi yake kwa idara ya mahakama kutokana na uamuzi wa kuharamisha mswada huo.

“Mahakama ilipaswa kujiuliza manufaa kwa mwananchi yatakayojiri kupitia BBI, ambao ni mswada wenye maoni ya Wakenya. Inapaswa kuheshimu sauti ya wananchi,” kiongozi wa nchi akaelezea, akifufua makovu ya 2017, mahakama ya juu zaidi ilipofutilia mbali ushindi wake.

Aidha, baada ya ushindi wa Rais Kenyatta na naibu wake, Dkt William Ruto, 2017 kuharamishwa na uchaguzi mpya wa kiti cha urais kuandaliwa, aliapa kutathmini utendakazi wa idara ya mahakama, kilele kikiwa kupunguza mgao wa fedha kwa idara hiyo.

Hadi kustaafu kwake, Jaji Mkuu (CJ) David Maraga alilalamikia idara ya mahakama kukandamizwa na afisi ya rais.

Bi Martha Koome, ndiye aliteuliwa na kuapishwa kumrithi mnamo Mei 2021.

Huku Rais Kenyatta akikosoa uamuzi wa mahakama kuu, pamoja na Bw Odinga wametangaza kukata rufaa ya uamuzi wa mahakama kuu.

  • Tags

You can share this post!

Mfumaji Mason Greenwood ajiondoa kwenye timu ya taifa ya...

Beki Eric Garcia abanduka Man-City na kutua Barcelona kwa...