• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 2:31 PM
Waislamu North Rift wasisitiza ni sharti Mentor ifungwe kwa kuwavunjia heshima

Waislamu North Rift wasisitiza ni sharti Mentor ifungwe kwa kuwavunjia heshima

NA TITUS OMINDE

BARAZA la Maimamu na Wahubiri (CIPK) North Rift limetangaza litaendelea kufanya maandamano kila siku kushinikisha kufungwa kwa kampuni iliyochapisha picha ya kumsawiri Mtume Muhammad katika sehemu ya Somo la Dini ya Kiislamu (IRE).

Mwenyekiti wa CIPK North Rift alisema licha ya kampuni husika kuomba msamaha, serikali inapaswa kufunga kampuni hiyo.

Kwenye kitabu hicho cha ‘Grade 2 Mentor Encyclopedia’ cha Mentor Publishing Co LTD, kuna mchoro unaosawiri Mtume Muhammad na maelekezo kwa wanafunzi wa somo la IRE kuupaka rangi.

“Licha ya kuomba msamaha na kuondoa sokoni kitabu hicho, kampuni hiyo inapaswa kufungwa mara moja. Sisi Waislamu tunaheshimu maadili na hutungependa maswala ya dini kufanyiwa mzaha,” alisema Sheikh Bini.

Sheikh Bini alisema iwapo kampuni hiyo haitafungwa, Waislamu katika mji wa Eldoret watakuwa wakifanya maandamano kila baada ya ibada.

“Serikali inapswa kutilia maanani kilio chetu kwamba ni lazima kampuni hiyo ifungwe mara moja la sivyo tutafanya maandamano kila wiki,” alisema Sheikh Bini.

Msimamo sawa na huo umetolewa na wazazi katika shule mbalimbali mjini Eldoret.

Kuwepo kwa mchoro huo kumelaaniwa na wazazi wengi wenye kufuata dini ya Kiislamu.

Tayari mchapishaji huyo ameomba msamaha na kulazimika kuagiza vitabu vyote kwenye soko virudishwe kwa kampuni hiyo ili “turekebishe mambo.”

  • Tags

You can share this post!

Wanaokalia dhahabu eneo la Ramula kuhamishwa

Mkenya kizimbani kwa kumlaghai raia wa Rwanda Sh390 milioni

T L