• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 4:55 PM
Waislamu wamlilia DCI akomeshe utekaji

Waislamu wamlilia DCI akomeshe utekaji

Na WINNIE ONYANDO

VIONGOZI wa dini ya Kiislamu Ijumaa waliwasilisha malalamishi kwa ofisi ya Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Makosa ya Jinai (DCI) wakiomba serikali iingilie kati kukomesha utekaji nyara na kuuawa kwa watu.

Wakiongozwa na mwenyekiti wa Baraza Kuu la Viongozi wa Waislamu, Al-Hajj Hassan Ole Naado, viongozi hao walidai kuwa watu wa dini ya Kiislamu wamekuwa wakitekwa nyara kila mara bila serikali kuchukua hatua yoyote.

“Serikali haifai kukichukulia kikundi kimoja cha dini kuwa na hatia. Sheria inasema kuwa kila mmoja ana haki ya kulindwa na serikali . Tunaomba haki itendewe familia za waathiriwa,” akasema.

You can share this post!

Hatari Afrika ikipunguziwa chanjo ya corona hadi nusu

Serikali yabuni kaunti ndogo mpya