• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 11:59 AM
Wito watu wapime kansa ili kupunguza ada za kutibu

Wito watu wapime kansa ili kupunguza ada za kutibu

Na JUMA NAMLOLA

WAKENYA wameshauriwa wapime kama wana kansa au la, ili kupunguza gharama za matibabu kwa kuanza tiba mapema.

Mwenyekiti wa Jopo Maalumu kuhusu Kansa, Dkt Mary Nyangasi, anasema watu wengi hujipeleka hospitalini ugonjwa wa kansa unapokuwa katika hatua za mwisho, ambapo huwa vigumu kuutibu.

“Kansa ina tiba, hasa inapokuwa katika awamu ya kwanza au ya pili. Watu wengi hukosa kuzitambua dalili na mapema. Wanapofika hospitalini, huhitaji mamilioni kutibu kansa inapokuwa imezagaa mwilini,” akasema Dkt Nyangasi jana Jumanne kwenye mkutano na wanahabari katika hoteli ya Serena, Nairobi.

Baadhi ya dalili za kansa ni sawa na za maradhi mengine. Kufanya malengelenge, kikohozi kisichoisha, kupungua uzani wa mwili, kubadilika mfumo wa kwenda haja kubwa na kadhalika.

Mkurugenzi wa Baraza la Vyombo vya Habari (MCK) anayesimamia utoaji mafunzo, Bw Victor Bwire, aliwapa changamoto wanahabari waifanye kansa kuwa mada kuu kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu ujao.

“Naomba wanahabari tuwashinikize wanasiasa waeleze sera zao kuhusiana na kanasa,” akasema Bw Bwire.

You can share this post!

CECIL ODONGO: ODM isipotoshwe mkono wa Rais ushafikisha...

Ghana kuwapiga faini wanaosafiri huko bila vyeti

T L