• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 2:31 PM
Aliachwa akakataa kuachika, sasa kijana Naftali Kinuthia ataona nje ya jela akiwa mzee wa miaka 73

Aliachwa akakataa kuachika, sasa kijana Naftali Kinuthia ataona nje ya jela akiwa mzee wa miaka 73

NA TITUS OMINDE

Naftali Kinuthia, 33, aliyepatikana na hatia ya kuua mpenzi wake baada ya kutoalikwa kwa sherehe ya siku ya kuzaliwa, Alhamisi Desemba 14, 2023 amefungwa jela miaka 40 kwa kosa hilo.

Jaji Stephen Githinji alisema kwenye uamuzi wake kwamba, kutoalikwa kwenye sherehe kama hiyo haikuwa sababu tosha ya kumuua mpenzi.

Kwenye tukio hilo mwaka 2019, Kinuthia alifika nje ya kitivo cha utabibu cha chuo kikuu cha Moi mjini Eldoret akiwa na shoka.

Wakati wa kujitetea kortini, Kinuthia alisema wakati mmoja alitumia zaidi ya Sh200,000 kwa Ivy Wangeci, ambaye walikuwa marafiki tangu utotoni walipokuwa shule ya msingi moja mjini Thika.

Aliendelea kumfadhili Wangeci hata baada ya kuwa mbali naye.

Aliambia mahakama kuwa, alipatwa na hasira alipoona mpenzi wake akikumbatia mwanaume mwingine. Alikasirika kuwa Bi Wangeci aliendelea kukusanya pesa kutoka kwake, ilhali hakuwa na nia ya kuendelea na uhusiano wa kimapenzi na yeye.

Alimwambia Jaji Githinji kwamba, kabla ya kuchukua uamuzi wa kumuua, alikuwa amemtumia Sh7,000 kwa siku yake ya kuzaliwa, lakini hakuwa amemwalika kwenye sherehe.

Hakukasirika, alisema, kwa sababu amekuwa akimfadhili kwa miaka mingi ili kulinda uhusiano. Kilichomuudhi ni Ivy kumkumbatia mwanaume mwingine mbele yake.

Kupitia kwa wakili wake, Wokabi Mathenge, mwanaume huyo alielezea kujutia kosa alilotenda, na kuiambia mahakama kuwa amebadilika kwa muda wa miaka minne aliyokuwa rumande.

Mwanume huyo, 33, alikamatwa baada ya kumshambulia kwa shoka mpenzi wake ambaye wakati huo walikuwa wameachana.

Kupitia kwa wakili wa familia Kiroko Ndegwa, familia ya marehemu ilikuwa imeomba mahakama kumwadhibu Bw Kinuthia kwa kifungo cha kunyongwa.

  • Tags

You can share this post!

Mwandishi mkongwe atuzwa kwa kusaidia umma kuelewa mchezo...

Mtaalamu: Ugumu wa maisha unavyoathiri ukuaji wa watoto...

T L