• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 10:50 AM
Mwisho wa mfumo wa 8-4-4 (KCPE), mwanzo wa KPSEA (CBC)   

Mwisho wa mfumo wa 8-4-4 (KCPE), mwanzo wa KPSEA (CBC)  

NA SAMMY WAWERU

SHUGHULI ya usambazaji wa mitihani ya Kitaifa ya Darasa la Nane (KCPE) na ya wanafunzi wa Gredi ya Sita (KPSEA), imeanza kote nchini maafisa wakuu serikalini wakiiongoza.

KCPE na KPSEA, watahiniwa wanaanza kuandika mitihani hiyo leo, Jumatatu, Oktoba 30, 2023.

Huku zoezi hilo likitarajiwa kuendelea kwa muda wa siku tatu zijazo, KCPE 2023 itakunja jamvi la mfumo wa 8-4-4 ulioanza 1985, na kubisha hodi mfumo mpya wa CBC.

Jumla ya watahiniwa 1,415,315 wanatarajiwa kufanya KCPE na KPSEA 1, 282,574.

Zifuazo ni picha za baadhi ya vituo vya kuhifadhi mitihani hiyo, chini ya ulinzi mkali wa maafisa wa usalama na ikifunguliwa kwa minajili ya kusambazwa shuleni.

Naibu Kamishna Kaunti Ndogo ya Kati Kisii, Wilberfoce Kilonzo akisambaza mitihani Kisii Mjini. PICHA|WYCLIFFE NYABERI
Usambazaji wa mitihani ya KCPE 2023 na KPSEA Kaunti Ndogo ya Chuka. PICHA|ALEX NJERU
Usambazaji wa mitihani ya KCPE 2023 na KPSEA Kaunti Ndogo ya Chuka. PICHA|ALEX NJERU
Maafisa wa usalama wakilinda kituo cha kusambaza mitihani ya KCPE 2023 na KPSEA Kapenguria. PICHA|OSCAR KAKAI

Maafisa wa usalama wakilinda kituo cha kusambaza mitihani ya KCPE 2023 na KPSEA Kapenguria. PICHA|OSCAR KAKAI

  • Tags

You can share this post!

Punguzeni kununua nguo, mnazotupa kiholela zinachangia...

Mitihani ya KCPE 2023 na KPSEA yaanza kote nchini

T L