• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 8:50 AM
Rais Ruto amteua James Tembur kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NYS

Rais Ruto amteua James Tembur kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NYS

NA LABAAN SHABAAN

RAIS William Ruto amemteua James Kipsiele Tembur kuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Huduma ya Vijana kwa Taifa (NYS) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Desemba 20, 2023.

Haya ni kwa mujibu wa Gazeti Rasmi la Serikali ambapo Rais alisema: “Nikitekeleza mamlaka niliyopewa na sehemu ya 16 (1) ya Sheria ya 1 ya NYS, William Samoei Ruto, Rais wa Jamhuri ya Kenya na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, ninamteua James Kipsiele Tembur kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NYS kwa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia Desemba 20, 2023.”

Bw Tembur aliwabwaga Mbw Njiri Nelson Mugweru, Anjere Alfred Tom, Nakitari Humphrey Okuku, na Mbaruku Moses Njeru na kutwaa nafasi hiyo.

Waliomezea mate kiti hicho walifanyiwa usaili wa kazi mnamo Desemba 4, 2023, katika makao makuu ya NYS Nairobi.

Bw Tembur amekuwa akihudumu wadhifa huu akiwa kaimu baada ya kupokezwa mikoba ya uongozi na Bi Matilda Sakwa aliyekamilisha kipindi chake cha kuhudumu mnamo Aprili 2023.

  • Tags

You can share this post!

Malawi yakataa mahindi kutoka Kenya

Polo abaki singo tena kidosho akihepa kulishwa sukumawiki...

T L