• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 9:16 PM
Malawi yakataa mahindi kutoka Kenya

Malawi yakataa mahindi kutoka Kenya

NA LABAAN SHABAAN

MAHINDI kutoka Kenya yamepigwa marufuku kuingia Malawi licha ya taifa hilo kukumbwa na uhaba wa chakula.

Wizara ya Kilimo nchini humo imetangaza kuwa wanachukua tahadhari kuzuia uwezekano wa kusambaa kwa ugonjwa wa kugeuza mahindi kuwa manjano maarufu kama maize lethal necrosis disease (MLND).

Taarifa ya serikali hiyo imesema maradhi haya yanaweza kusababisha hasara ya mavuno kufikia kiwango cha asilimia 100.

Mamlaka ya Kilimo ya Malawi inasema maradhi hayo ya mimea hayana tiba na watanunua bidhaa ya mahindi ikiwa imechakatwa na kusagwa na kuwa unga kuepuka msambao nchini humo.

Kadhalika, Malawi imepiga marufuku mahindi kutoka taifa jirani la Tanzania kwa sababu iyo hiyo.

Kwa muda sasa, nchi hizi mbili, Kenya na Tanzania, zimekuwa vyanzo vya mahindi kwa Malawi katika vipindi vya uhaba wa chakula.

Taifa hilo linakumbwa na uhaba wa chakula baada ya kimbunga Freddy kuharibu maelfu ya hekta za mahindi mnamo Machi 2023.

Ili kukidhi mahitaji ya mahindi, Malawi itaelekea nchini Afrika Kusini ambapo inatazamia kugharamika zaidi kwa sababu ya umbali.

Haya ni kwa mujibu wa Rais wa Muungano wa Wafanyabiashara wa Nafaka nchini Malawi Grace Mijiga.

Ugonjwa huu wa mahindi (MLND), unaibuka na kuwa hatari kwa uzalishaji wa mahindi Kenya na katika nchi jirani.

MLN husababisha hasara kati ya asilimia 30 hadi 100 shambani mlimopandwa mihindi.

Kwa sasa, athari kubwa zinashuhudiwa kaunti za Embu, Uasin Gishu, Nakuru, na Elgeyo Marakwet.

Kwa mujibu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) mahindi huchangia asilimia 85 ya mimea ya nafaka inayokuzwa nchini.

  • Tags

You can share this post!

Warembo wa tattoo wadai ni vigumu kupata mume

Rais Ruto amteua James Tembur kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NYS

T L