• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 10:50 AM
Waajiri waliwapuuza wafanyakazi wakati mgumu wa Covid-19

Waajiri waliwapuuza wafanyakazi wakati mgumu wa Covid-19

IDADI kubwa ya wafanyakazi nchini walihisi kwamba waajiri wao hawakuwasaidia wakati wa janga la Covid-19, kulingana na Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu (KNCHR).

Hayo ni kwa mujibu wa wafanyakazi waliodumisha kazi zao baada ya wenzao milioni mbili kupoteza ajira, tangu ugonjwa huo uliporipotiwa nchini mnamo Machi 13, 2020.Jumla ya watu milioni 10 waliathirika moja kwa moja na janga hilo.

Katika ripoti hiyo iliyotolewa na KNCHR mjini Eldoret, asilimia 80 ya wafanyakazi walihisi kutelekezwa na waajiri.Ni asilimia 19.8 pekee waliohisi kwamba waajiri wao waliwasaidia wakati wa makali ya Covid-19.“Wafanyakazi walihisi kwamba waajiri wao hawajawasaidia inavyopasa katika kipindi hiki cha janga la Covid-19 tangia Machi 15,2021,” sehemu ya ripoti hiyo inasema.

“Wengi pia hawakufahamu maana ya kufanya kazi kutoka nyumbani,” akaongeza Dkt Benard Mogesa, Afisa Mkuu Mtendaji wa KNCHR. Wafanyakazi wanaoishi mijini waliogopa kwenda maeneo ya mashinani kwa hofu wangeadhibiwa na waajiri wao.

Baadhi ya wafanyakazi walilalamika kwamba wanadhulumiwa na waajiri wao,” akasema Dkt Benard Mogesa, Afisa Mkuu Mtendaji wa KNCHR.Ripoti hiyo pia inasema kuwa kulikuwa na ongezeko la idadi ya watu waliotegemea usaidizi wa watu walioajiriwa hasa walimu na watumishi wa umma.

You can share this post!

Mahakama yasimamisha mazishi ya watu 5 waliouawa kinyama

Maelfu wakesha katika uwanja wa Kasarani

T L