• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:55 AM
Mwimbaji bingwa ‘General Defao’ 62, aaga dunia

Mwimbaji bingwa ‘General Defao’ 62, aaga dunia

Na PATRICK ILUNGA,

DR CONGO

MWANAMUZIKI maarufu mzaliwa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Lulendo Matumona, maarufu kama, General Defao ameaga dunia, akiwa na umri wa miaka 62.

Alifariki Jumatatu jioni jijini Douala, Cameroon, ambako amekuwa akishiriki tamasha mbalimbali msimu huu wa sherehe.

Familia yake, ikithibitisha kifo chake, ilisema afya yake ilikuwa imedhoofika kwa muda mrefu lakini ikakataa kufichua chanzo cha kifo chake.

Katika miaka ya 1990, General Defao aliondoka nchini DRC na kuamua kuishi Kenya huku uvumi ukienea kuwa alisaka uhifadhi wa kisiasa.

Hata hivyo, aliporejea nchini DRC Agosti 2019, mwanamuziki huyo alikanusha madai kuwa kuishi kwake uhamishoni kwa zaidi ya miaka 15 kulihusiana na siasa.

Lakini kulingana na wachanganuzi wa kisiasa nchini DRC, mwanamuziki huyo alikuwa mpinzani mkubwa wa rais wa zamani wa nchi hiyo Joseph Kabila.

Defao alizaliwa Desemba 31, 1959.

Alianza shughuli za muziki 1976 akiwa na umri wa miaka 17 pekee.

Mnamo 1981, alijiunga na bendi ya Grand Zaiko Wawa iliyoongozwa na mcharaza gita mashuhuri Pepe Felly Manuaku.

Baadaye 1983, Defao aligura bendi hiyo na kujiunga na bendi ya Choc Star iliyooongozwa na Ben Nyamabo.

Aliimba akishirikiana na wanamuziki maarufu kama vile Bozi Boziana, Lassa Carlyto, Debaba, Djuna Djanna, Nzaya Nzayadio.

Ilipotimu 1991, alianzisha bendi ya Big Star Orchestra na hapo ndipo umaarufu wake ulianza kuenea kutokana na vibao kadha alivyofumua jijini Paris, Ufaransa.

Katikati mwa 2000, bendi ya Big Star Orchestra ilikabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za kiusimamizi, hali iliyochangia wanamuziki wake kutapakaa kote ulimwenguni.

General Dafao alirejea Afrika na kupiga kambi haswa nchini Kenya.Baadaye alirejea DRC na kujaribu kuzindua upya muziki wake na amekuwa akifanya shoo mbalimbali katika mataifa kadha Afrika Mashariki na Kati.

  • Tags

You can share this post!

Mvamizi Ferran Torres ajiunga na Barcelona

CECIL ODONGO: Oburu apewe useneta lakini si kwa sababu ya...

T L