• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 9:50 AM
Putin awazia kutumia ‘silaha zisizo za kawaida’ vitani

Putin awazia kutumia ‘silaha zisizo za kawaida’ vitani

VOLOGRAD, URUSI

RAIS Vladimir Putin wa Urusi amesema kuwa historia inajirudia katika vita vinavyoendelea baina nchi yake na Ukraine, kwani kwa mara nyingine inajipata ikikabiliana na Ujerumani.

Hapo jana, Putin alifananisha uvamizi wa Ukraine na juhudi zake kukabili utawala wa Nazi nchini Ujerumani miaka 80 iliyopita.

Putin alitoa kauli hiyo kwenye hotuba aliyotoa kuadhimisha kukamilika kwa Vita vya Stalingrad.

Ujerumani ni miongoni mwa nchi kadhaa ambazo zimeamua kuisaidia Ukraine kwa silaha ili kuitetea himaya yake.

Akihutubu katika eneo la Volgograd—jina jipya la Stalingrad—Putin alisema huenda akalazimika kutumia silaha zisizo za kawaida.

“Wale wanaotarajia kuishinda Urusi kwenye vita hivi hawaelewi. Inaonekana vita vya kisasa baina yao na Urusi vitakuwa tofauti sana,” akasema.

Akaongeza: “Hatutumi vifaru vyetu katika mipaka yao, japo tuna njia ya kujibu mashambulio yao. Si lazima tutumie njia za kawaida. Lazima kila mmoja aelewe hili.”

Msemaji wa serikali Dmitry Peskov alikataa kutoa ufafanuzu kuhusu matamshi ya Putin.Putin alikuwa katika eneo la Volograd kuadhimisha mwisho wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, ambapo majeshi ya Muungano wa Usovieti (USSR) yalifanikiwa kuwateka wanajeshi karibu 91,000 wa Ujerumani.

  • Tags

You can share this post!

Petanns yafungua chuo cha kiufundi kuwasaidia vijana kupata...

Raila atorokwa na wandani wa karibu

T L