• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 8:50 AM
KIKOLEZO: Wenzetu waliamua kwa dhiki au faraja

KIKOLEZO: Wenzetu waliamua kwa dhiki au faraja

Na THOMAS MATIKO

TUKIWA bado kwenye ile mudi ya funga mwaka, tunazidi kukumbushana tu matukio yaliyoyojiri 2021.

Ukiachia mbali maceleb tulioshuhudia wakiachana, pia tulishuhudia baadhi yao wakivishana pingu za maisha.

Kwa dhiki au kwa tabu, kwa raha au karaha. Hebu wacheki hawa:

Nyash au ukipenda mwite Ganzee, unaweza kusema jamaa anajua kujipanga. Alianza kwa kuchumbia demu wake wa muda mrefu Zia Bett.

Kisha akafanya ile sherehe ya kutoa mahari ruracio Novemba 2019 kule kijijini kwa kina binti Itigo, Kaunti ya Nandi.

Halafu mwaka uliofuatia, akacheza kama yeye na wakabarikiwa kupata mtoto wao wa kwanza.

Na sasa mwaka huu 2021, waliamua kuumaliza kwa kufunga ndoa chini ya maji wiki iliyopita. Ndoa hiyo ilihudhuriwa na watu wa karibu wa Nyash kama vile staa Nameless, Robert Burale, Big Pin, DJ Stylez, Collo, Wahu huku meneja wake wa zamani Fakii Liwali akiwa mshereheshaji wa hafla hiyo.

Reverendi Nick Korir ndiye aliyewafungisha ndoa hiyo katika kanisa la Nairobi Chapel. Tunawaombea mema.

ANITA NDERU NA BARRETT RAFTERY

Baada ya uhusiano wa miaka saba na mpenzi wa Kihindi Sun Man, mambo yalienda segemnege na wawili hao wakaachana.

Anita alihakikisha kuwa kuachana kwao imesalia kuwa siri kama kifo. Hakuna aliyefahamu kuwa mrembo huyo mtangazaji alikuwa amerudi sokoni, hadi mwaka 2020 alipofichua yeye mwenyewe.

Lakini taratibu akajinyakia mzungu kutoka Marekani ambaye naye alitimiza wajibu wake kwenye sherehe ya ruracio na baada ya wiki mbili Septemba ya mwaka huu 2021, wakafunga ndoa.

Ndoa hiyo ilifanyika kwenye hoteli ya kifahari ya nyota tano maeneo ya Nanyuki. Wageni waalikwa walikuwa maceleb na watu wa karibu wa Anita kama vile mwigizaji Sarah Hassan, Amina Abdi Rabar, Joe Muchiri kati ya wengine.

MOJI SHORT BABA NA NYAWIRA GACHUGI

Mzee wa ‘Vimbanda’ baada ya kuwa na binti wa watu aliyekutana naye kanisani kwa miaka mitatu, aliamua kuhalalisha mambo.

Alianza kwa kufunga ndoa ya kitamaduni na Mei 1, 2021 wakafunga ndoa yao rasmi.

Moji alihakikisha ndoa yake inafanyika chini ya maji. Nilipopiga stori naye kipindi hicho na kutaka kujua ni kwa nini hakualikana, jamaa aligeuka mbogo.

“Kazi yangu ni kuimba na ndicho watu wananifahamu nacho. Masuala ya maisha yangu huwa sipendi kuyaweka hadharani. Ningeifanya hadharani wapo watu wangelalamika sikuwaalika,” akasema.

Moji anasema alifanya kusudi la kutowaalika watu wengi wa karibu ili asionekane mbaguzi.

MODO MOKORINO PESH NA DAN MAGENDA

SIKU hizi tunaishi kwa kasi ya 4G. Wapo mamodo wa Kikorino ambao nao wameamua kufanya yao licha ya kukaziwa maisha na dini.Mmoja wa mamodo hao wa Kikorino ni Pesh ambaye alifunga ndoa Novemba mwaka huu na mchumba wake Magenda.

Ilikuwa ndoa ya chini ya maji iliyohudhuriwa na wanafamilia wa Pesh wengi wakiwa ni wadau wa dhehebu lake. Wengine sisi tulijulia mitandaoni baada ya yeye kuposti.

JAYMO ULE MSEE NA CATHERINE WAKIO

Mwenyekiti huyu wa Team Mafisi, alihalalisha uhusiano wake na mpenzi wake wa muda mrefu Wakio, Septemba 25.

Ndoa yao haikuwa ya kanisani ila ya kitamaduni kwa mujibu wa mila na desturi za Agikuyu.

Kabla ya ndoa, walichumbiana kwa miaka miwili baada ya Jaymo kumposa kwenye sherehe ya Valentine Dei walipokuwa likizoni Maasai Mara.

Wakio na Jaymo walikutana 2015 kwenye mishe mishe zao za maigizo.

GLORIA MULIRO NA EVANS SABWANI

Baada ya ndoa yake kuvunjika miaka sita iliyopita, nyota wa injili Muliro alimpata mpenzi mwingine, Sabwami aishiye Marekani.

Taarifa hizi alitufahamisha Muliro Februari 14 kwenye siku ya wapendanao. Oktoba 2021, wakafunga ndoa kule New York iliyohudhuriwa na wanafamilia tu.

Mchekeshaji wa mitandaoni Kazungu naye alifunga ndoa na mpenzi wake Emcee Kibunja.

Ndoa yao ilifanyika Septemba na kuzua gumzo baada ya wanandoa hao kutumia bajeti ya Sh60,000 tu. Ndoa hiyo ilifungiwa kwenye afisi ya mwanasheria mkuu.

You can share this post!

Wawaniaji wa ugavana Bungoma njia panda kuhusu chama cha...

TUSIJE TUKASAHAU

T L