• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 5:50 AM
BORESHA AFYA: Faida za kiwano

BORESHA AFYA: Faida za kiwano

NA MARGARET MAINA

[email protected]

Kiwano huboresha usagaji wa chakula

Kiwano huwa na nyuzi ambazo huboresha mchakato wa kusaga chakula mwilini. Kazi kuu ya nyuzinyuzi ni kuwezesha mmeng’enyo wa chakula. Husaidia kuzuia magonjwa kadhaa kama saratani ya koloni na vidonda vya tumbo na kusafisha njia ya mkojo.

Hupunguza uzee wa mapema

Kiwano hutoa vitamini C, husaidia katika uzalishaji wa collagen – kolajeni – na kurekebisha ngozi iliyoharibiwa na tishu za kiungo. Virutubisho ndani ya tunda hili hulinda seli kutokana na majeraha, sumu na bidhaa za taka ambazo zinaweza kusababisha matatizo mengi ya kuzeeka. Zaidi ya hayo, matumizi ya mara kwa mara ya kiwano huzuia dalili za awali za kuzeeka, kama vile makovu na madoa.

Hupunguza mafadhaiko

Kiwano husaidia kudhibiti homoni za mafadhaiko, kama vile adrenaline. Watu ambao wanakabiliwa na wasiwasi wa muda mrefu wanaweza kula kiwano kwa sababu ni kitulizo kamili.

Hudumisha mchakato wa kimetaboliki

Kwa kuwa mchakato wa kimetaboliki huvunja chakula, mwili unahitaji vipengele muhimu ili kufanya kazi zake vizuri. Kiwano hutoa kiasi cha kutosha cha zinki inayohitajika pakubwa wakati wa kutoka kwa insulini na mchakato wa kawaida wa kimetaboliki ya vyakula vya wanga. Pia huzalisha seli za damu na husaidia kurekebisha majeraha.

Huboresha kuona

Kiwano huwa na kiasi kikubwa cha vitamini A ambayo husaidia kuboresha macho yako. Vitamini A huzuia kuzorota kwa nguvu ya macho kuona na pia huondoa itikadi ambayo husababisha muwasho wa macho na shida mbalimbali za macho.

Huimarisha mifupa yako

Kiwano huwa na madini mbalimbali kama zinki, kalsiamu na madini mengine. Madini haya husaidia katika ukuaji wa mifupa. Kwa sababu ya uwezo wake wa kuhifadhi kalsiamu, kiwano ni muhimu kwa walio na matatizo mbalimbali ya mifupa.

Kuimarisha nywele

Kipengele cha lishe kwenye tunda la kiwano kinaweza kuboresha nguvu za nywele zako na kuzifanya kuwa na rutuba.

Hupunguza hatari ya kunenepa kupita kiasi

Maji yaliyomo kwenye kiwano husaidia kuondoa vitu vyenye madhara kutoka kwa mwili wako. Jambo la kutia moyo zaidi ni kwamba si lazima uweke kikomo ulaji wako wa kiwano.

  • Tags

You can share this post!

Wataalamu na wasomi wa Kiswahili watathmini maendeleo yake...

Uhuru achomoa minofu kuzolea Raila kura urais

T L