• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 7:50 AM
Faida za mbegu za mpopi

Faida za mbegu za mpopi

NA MARGARET MAINA

[email protected]

MBEGU za mpopi ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi muhimu kwenye lishe.

Nazo husaidia ujisikie umeshiba kwa muda mrefu. Pia mbegu hizi zina kiwango cha juu cha magnesiamu, madini ambayo ni muhimu kwa afya nzuri ya mifupa na kuganda kwa damu. Nayo madini ya chuma na kalsiamu kwenye mbegu za mpopi yana jukumu kubwa katika maendeleo na afya ya mfumo wa neva.

Baadhi ya faida maarufu za mbegu za mpopi ni kama vile:

Kupambana na tatizo la kukosa usingizi

Mpopi ni mzuri katika kusaida kupata usingizi kwa sababu hufanya kazi kama kitulizo. Mbegu hii husaidia katika kuleta chini viwango vya mkazo. Unaweza kutayarisha na kunywa kama chai au utengeneze mbegu hizi ziwe unga kisha uchanganye na maziwa.

Nguvu ya mifupa

Kwa kuwa zina madini mengi ya shaba na kalsiamu, mbegu za mpopi husaidia kuboresha afya ya mifupa. Manganisi katika mbegu hizi husaidia katika utengenezaji wa protini aina ya collagen ambayo hulinda mifupa kutokana na uharibifu mkubwa.

Huboresha usagaji chakula

Mbegu za mpopi ni chanzo kikubwa cha nyuzinyuzi zinazosaidia katika kuimarisha mfumo wa usagaji chakula na kutibu kuvimbiwa kwa tumbo.

Husaidia kuimarisha afya ya moyo

Mbegu za mpopi zina nyuzi nyingi ambazo ni sehemu muhimu ya lishe na hupunguza viwango vya lehemu hatari mwilini na kuweka viwango vya lehemu nzuri juu. Mbegu za mpopi pia zina utajiri wa madini ya chuma na huboresha mzunguko wa damu. Viwango vya shinikizo la damu hudhibitiwa kwa matumizi ya mbegu za mpopi. Mbegu hizi pia zina asidi ya mafuta ya Omega-3 ambayo ni ya manufaa katika kupunguza uwezekano wa magonjwa ya moyo na mishipa.

Huimarisha mzunguko wa hewa safi mwilini na kufanya ubongo kufanya kazi vizuri

Mbegu za mpopi ni matajiri katika chuma. Hii husaidia kusafisha damu na kuongeza viwango vya hemoglobini katika damu. Ulaji wa mbegu za mpopi unaweza kusaidia kuboresha mzunguko wa damu ambao husababisha ugavi bora wa oksijeni kwa kila sehemu ya mwili ikiwa ni pamoja na ubongo wako.

  • Tags

You can share this post!

Faida za mkaa

BENSON MATHEKA: Magavana wasifute kazi wafanyakazi kwa...

T L