• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
Farasi wanaokula biskuti na kaimati kabla ya kula nyasi

Farasi wanaokula biskuti na kaimati kabla ya kula nyasi

NA FRIDAH OKACHI

MFUGAJI wa farasi Mohamed Wangusi mjini Bungoma, anamiliki farasi watatu waliokuwa wakitumiwa na Malkia Elizabeth.

Farasi hao wanatumika kwenye mapambo ya harusi na sherehe za kuzaliwa pamoja na kuvuta gari la jeneza nchini Kenya. Malipo kwenye biashara hiyo ikiwa ni Sh1.2 milioni kwa kila sherehe.

Mwazilishi huyo wa Royal queens carriage, aliambia Taifa Leo aliuziwa farasi hao na Mfalme Charles III, kutoka kwa shamba la Malkia Elizabeth huko Uingereza.

 “Tulitumia pesa ambazo unaweza kununua V8, tulitumia zaidi ya milioni tatu kwa farasi mmoja. Kabla wafike hapa walikaa kwenye uwanja wa ndege kwa miezi sita. Pia, walitupa daktari ambaye alikuwa akiwaangalia,” alisema Bw Wangusi.

“Tunalo jina katika himaya ya Uingereza. Hivi sasa wana mpango wa kutuuzia farasi wawili wa kike. Tuna farasi wa dume mmoja anafahamika Stallion aliyekuwa akitumiwa na malkia huyo,” aliongezea.

Mfanyabiashara huyo amesema kabla ya kuanza kufuga farasi hao, walilazimika kujenga nyumba wanamoishi mara tatu.

“Tulibomoa nyumba hiyo mara tatu, hao farasi wakija wasione wanabadilishiwa mazingira, walitaka nyumba kama ile waliyokuwa wakiishi. Pia walitaka kuona iwapo tutaweza kumudu na kulazimika kununua chakula cha miezi sita,” asimulia.

Kando na kula nyasi, farasi hao hula vitafunio aina ya biskuti na kaimati.

“Hawa farasi wanakula vitafunio vya biskuti, kaimati na maji kabla ya kula chakula kingine,” alisema mwazilishi huyo.

Farasi hao ambao wana upekee wa kuwa na nguvu, weupe na wakubwa kupita kiasi, wanakula chakula kutoka ng’ambo, kila siku gharama ya mmoja ikiwa ni Sh50,000.

“Kila siku wanachanwa nywele na kupakwa mafuta. Kando na vitafunio, wanakua nyasi aina ya Bomroad na arushwa kilo 20 kila mmoja. Nyasi hiyo ikiuzwa Sh400,” alielezea.

Bw Wangusi alisema kuwepo na uhaba wa farasi barani Afrika ndio sababu ya ufugaji huo ili kuwapa Wakenya nafasi ya huduma za farasi waliowekwa katika himaya ya kifalme mjini Nairobi, Bungoma na Nakuru.

  • Tags

You can share this post!

Wakenya walio na ghadhabu watajia Serikali huduma zaidi za...

Tambua kwa nini demu shabiki sugu wa Messi ‘Miss...

T L