• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 8:55 AM
Jinsi ya kuandaa pilau ya nyama ya mbuzi

Jinsi ya kuandaa pilau ya nyama ya mbuzi

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kufanya matayarisho: Dakika 15

Muda wa mapishi: Saa 1

Walaji: 5

Vinavyohitajika

  • mchele wa Basmati vikombe 3
  • nyama ya mbuzi kilo 2
  • viazi 3
  • vitunguu 5 (vikatakate)
  • kitunguu saumu kilichosagwa vijiko 2
  • bizari ya pilau nzima vijiko 3
  • mdalasini
  • pilipili manga chembe kiasi
  • karafuu nzima chembe 7
  • hiliki chembe 7
  • chumvi kiasi
  • mafuta ya kupikia kikombe ΒΌ

Maelekezo

Osha mchele na uloweke.

Changanya nyama na chumvi na tangawizi kisha chemsha nyama kwa maji kiasi vikombe sita. Ikishaiva weka kando, na itabakia supu yake kiasi.

Weka mafuta katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vikaribie kugeuka rangi.

Tia vipande vya viazi ukaange kidogo.

Tia bizari nzima, pilipili manga, karafuu, na kijiti cha mdalasini.

Pondaponda hiliki kisha uendelee kukaanga kidogo tu.

Mimina mchele, kaanga kidogo, kisha mimina nyama na supu yake na uhakikishe unatumia maji kiasi cha vikombe tano.

Koroga kisha funika halafu upike pilau kwa moto wa wastani kiasi hadi iive.

Pakua na ufurahie.

You can share this post!

Wakenya wengi hawataki BBI – Utafiti

RIZIKI: Ushonaji nguo unahitaji utafiti wa kutosha kuelewa...