• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 5:50 AM
Wakereketwa wa Kiswahili wamuenzi mwenzao Kericho kwa mchango wake katika lugha

Wakereketwa wa Kiswahili wamuenzi mwenzao Kericho kwa mchango wake katika lugha

NA WANTO WARUI

Chama Cha Wakereketwa wa Kiswahili kinachoitwa ‘NIENZI NINGALI HAI’ hapo jana kilimtembelea mmoja wao katika sehemu za Fort Tenan Kericho ili kumuenzi angali bado hai.

Mzee Thomas Koskei, ambaye pia ni mshairi maarufu nchini alipata fursa ya kuenziwa na wenzake kwa sababu ya mchango wake wa kukikunza Kiswahili kupitia mashairi yake tangu miaka ya themanini.

Akiongea katika kongamano hilo lililohudhuriwa na watu takriban 100, mwenyekiti wa chana hiki Bw Hassan Muchai alimpongeza sana Bw Koskei kwa kujitolea kwake katika Kiswahili licha ya umri wake mkubwa.

Bw Muchai alielezea umuhimu wa kuenziana watu wakiwa hai badala ya kusubiri kumtolea sifa tele mtu anapokufa. Alielezea hatua ambazo chama kimepiga tangu kilipoanzishwa mwaka wa 2005 ambapo kilimuenzi marehemu Mwalimu Hassan Mbega kwake nyumbani eneo la Masinga.

Pamoja na kumuenzi Bw Koskei, pia kulikuwa na uzinduzi wa diwani yake ya mashairi iliyoitwa ‘Lugha Naishangilia’ iliyochapishwa na kampuni ya Mjikeo Communications Limited.

Waliohudhuria kongamano hilo ni pamoja na katibu wake Henry Indindi, Andrew Watuha, Mwenyekiti wa WAKITA Dkt Abdul Noor, Kinyua King’ori, Wanto Warui, Mutribu mkongwe kutoka Mombasa Bi Zuhura miongoni mwa wengine.

Muuzaji maarufu wa gazeti la Taifa Leo eneo la Fort Tenan, Kericho Bi Emily Chepkurui ajumuika na mshairi mahiri Thomas Koskei wakati wa hafla ya kumuenzi Koskei iliyofanyika Novemba 25, 2023 kijijini Chilchila Koisagat, Kericho. Pamoja pichani Ni mwenyekiti wa WAKITA Abdul Noor na naibu wake Kinyua Kingori. PICHA|HASSAN MUCHAI

 

  • Tags

You can share this post!

Vijana wa Kenya waangushia Sudan kipigo kikali katika...

Wetang’ula ataka kaunti zitumie pesa kwa nidhamu ya...

T L