• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
Manufaa ya poda ya fenugriki

Manufaa ya poda ya fenugriki

NA MARGARET MAINA

[email protected]

MMEA wa fenugriki umekuwa ukitumika kwa muda mrefu kama dawa mbadala.

Ni kiungo cha kawaida katika vyakula vya Kihindi na mara nyingi huchukuliwa kama nyongeza. Inaweza pia kupatikana katika bidhaa, kama vile sabuni na shampoo.

Mimea hii inaweza kuwa na faida nyingi za kiafya kama vile;

Lishe

Mbegu za fenugriki zina sifa ya lishe yenye afya, iliyo na kiasi kizuri cha nyuzi na madini, ikiwa ni pamoja na chuma na magnesiamu.

Inaweza kusaidia kudhibiti ugonjwa wa kisukari na viwango vya sukari ya damu.

Fenugriki inaweza kusaidia michakato ya kimetaboliki, kama vile ugonjwa wa kisukari. Faida hizi zinaweza kuwa kutokana na jukumu la fenugriki katika kuboresha utendakazi wa insulin.

Hupunguza maumivu wakati wa hedhi

Ikiwa unapata maumivu kila wakati unapopata hedhi, jaribu kuwa na unga wa fenugriki. Gramu 2 hadi 3 za unga wa fenugreek katika siku tatu za kwanza za kipindi chako zinaweza kusaidia kupunguza maumivu kwa kiasi kikubwa.

Kupunguza uzito

Tumbo lenye afya humaanisha usagaji chakula bora, uvimbe mdogo, uondoaji wa sumu na udhibiti bora wa uzito. Kijiko kidogo cha poda ya fenugiki iliyochanganywa katika kikombe cha maji ya joto, inaweza kutumika kuzuia kuvimbia. Mbali na kuwa mmeng’enyo wa asili, unga wa fenugreek pia husaidia kutuliza tumbo na utando wa matumbo. Hii inapunguza asidi na kiungulia. Fenugriki pia huchochea kimetaboliki na kuunda joto katika mwili ambalo hukusaidia kuchoma mafuta kidogo zaidi unapofanya mazoezi.

Huimarisha unyonyeshaji

Ikiwa mama anayenyonyesha anakunywa chai iliyotiwa fenugriki, anaweza kutoa kiasi cha kutosha cha maziwa ya mama – chanzo bora cha chakula na virutubisho kwa mtoto mchanga.

Nzuri kwa moyo

Kwa kuweka usawa wa BP na lehemu, fenugriki imethibitishwa kusaidia afya ya moyo pia. Aidha, fenugriki pia hupunguza uwezekano wa atherosclerosis (kupungua na ugumu wa mishipa) ambayo inaweza kusababisha mshtuko wa moyo.

  • Tags

You can share this post!

MAPISHI KIKWETU: Jinsi ya kuandaa lasagna ya mboga mboga

BORESHA AFYA: Kukabili uvundo kinywani

T L