• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Mbinu mbalimbali za kuimarisha kinga mwilini

Mbinu mbalimbali za kuimarisha kinga mwilini

Na MARGARET MAINA

[email protected]

  • Mlo kamili

Lishe ya mimea inaweza kusaidia kuboresha kinga ya mwili. Mfumo wa kinga hutegemea seli nyeupe za damu zinazozalisha antibodies za kupambana na bakteria na hata virusi.

Kula lishe yenye mafuta kidogo kunaweza pia kuwa kinga. Kupunguza mafuta kwenye lishe husaidia kuimarisha kinga kwa sababu mafuta mengi kupindukia yanaweza kudhoofisha kazi ya seli nyeupe za damu.

Kunenepa sana kumehusishwa na hatari ya kuongezeka kwa mafuta na maambukizo mengine kama pneumonia. Lishe kutokana na mmea ni muhimu kwa kupoteza uzani kwa sababu ina utajiri wa nyuzi ambazo husaidia kukujaza, bila kuongeza kalori za ziada.

  • Fanya mazoezi

Mazoezi ya kawaida ni mojawapo ya nguzo za kuishi mtu akiwa na afya bora. Yanaboresha afya ya moyo na mishipa, hupunguza shinikizo la damu, husaidia kudhibiti uzani wa mwili na hulinda dhidi ya magonjwa. Mazoezi yanaweza kuchangia afya njema na kuimarisha mfumo wa kinga. Huimarisha mzunguko mzuri wa damu moja kwa moja.

  • Lala usingizi mzuri

Bila usingizi wa kutosha, tunaongeza hatari yetu ya kupata shida kubwa za kiafya kama ugonjwa wa moyo, ugonjwa wa Alzheimer, na kunenepa sana. Kulala bila kutosha pia kunahusishwa na kinga iliyokandamizwa. Ni muhimu kulala ili kupumzika.

Jaribu kuongeza matunda, mboga mboga, nafaka, na maharagwe kwenye lishe yako. Lishe iliyo na nyuzi nyingi na mafuta kidogo inaweza kusababisha upate usingizi mzito.

  • Usawa wa uzani na unene

BMI yako na ukubwa wa mwili, ni hesabu inayotumika kuamua ikiwa mtu ni mzito kupindukia au kadri. Ijapokuwa BMI sio kamili kwa sababu haionyeshi kiwango cha mafuta ya mwili, bado inachukuliwa kuwa njia mbadala ya kubaini watu ambao ni wanene sana au wakonde kupita kiasi, kwani kupima mafuta ya mwili moja kwa moja ni mchakato wa gharama kubwa.

Ikiwa BMI yako ni zaidi ya 25, kupunguza uzani ni wazo la busara.

  • Tags

You can share this post!

COPA AMERICA: Kiungo James Rodriguez atemwa kwenye kikosi...

Maafisa wapata ng’ombe kadhaa walioibwa kutoka Nakuru...