• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 2:29 PM
TALANTA: Hana mfano katika ufumaji

TALANTA: Hana mfano katika ufumaji

NA RICHARD MAOSI

WANAFUNZI wanaweza kutumia muda wao wa ziada kujifunza stadi kemkem tofauti na masomo ya darasani.

Hataua ya namna hii itawasaidia kuboresha kile wanachokifanya na kuwaepusha na utovu wa nidhamu. Hivyo basi, inashauriwa watumie wastani wa saa nane hivi shuleni.

Hali ni kama hiyo kwa Talib Lesaruni ambaye amejibidiisha kuweka mpangilio maalum wa mambo ya kufanya siku za wikendi na wakati wa mapumziko.

“Kwangu ni njia murua ya kupitisha muda ili kupunguza uchovu ikiwa ni baada ya kushinda kutwa nzima darasani,anasema.

Taifa Leo ilikutana naye majuzi katika hafla ya siku ya wazazi shuleni akijiandaa kunadi bidhaa zake kwa wazazi ambao walikuwa wakizuru wanao siku hiyo.

Lesaruni hutumia malighafi ya kawaida ya mkonge au nyasi kufuma vyombo kama vile uteo, mazulia na nembo za kutundika ukutani kwa ustadi wa hali ya juu.

Wanafunzi wenzake ndio mashabiki wake wakubwa hasa ikizingatiwa kuwa wamekuwa wakimsifu kwa kutengenezea nembo madhubuti, maridadi na za kuvutia.

Lesaruni anasema kwamba anatumai kuwa siku moja atakuja kufikisha sanaa yake mbali na hata aje kuwa balozi wa kutoa matangazo ya kibiashara kwa kampuni kubwa kubwa humu nchini.

Lesaruni anaongeza kuwa ni sanaa ambayo inamhimiza kuwa na maadili , bidii na uvumilivu kwani si rahisi kutengeneza bidhaa za maumbo ambayo yanakubalika na kupendwa na takriban kila mtu.

Talib mwenye umri wa miaka sita kutoka shule ya msingi ya Children of Freedom inayopatikana eneo la Lanet katika Kaunti ya Nakuru anasema kwamba lengo lake kuu katika elimu ni kuwa mhandisi katika siku za usoni.

Isitoshe, alijifunza namna ya kutengeneza aina tofauti za maumbo tangu akiwa shule ya chekechea, akizingatia ubunifu na maelekezo kutoka kwa mwalimu wake wa somo la sanaa.

“Aidha, huwa ninatumia muda mwingi kutazama vipindi vya watoto kwenye runinga, kushiriki katika michezo, upishi na hata kuangazia mazingira ninakoishi” asema.

Vilevile, anaungama kuwa maendeleo ya kihisisa na utambuzi yanamsaidia kufanya utafiti na kutambua mambo ambayo awali asingeweza kuyafanya kwa urahisi.

You can share this post!

MWALIMU WA WIKI: Theuri ni mwalimu mfano wa jungu kuu

Uhaba mkuu wa mafuta watatiza utoaji misaada

T L