• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 5:50 AM
Tatizo la tumbo kujaa gesi na jinsi ya kukabiliana na hali hiyo

Tatizo la tumbo kujaa gesi na jinsi ya kukabiliana na hali hiyo

Na MARGARET MAINA

[email protected]

TATIZO la tumbo kujaa gesi husababishwa na kumeza chakula pamoja na gesi inayotolewa katika vyakula mbalimbali tunavyovila na ambayo hujaa tumboni na kwenye utumbo mdogo.

Hali hii husababisha tumbo kujaa au kuvimba.

Nini husababisha hali hii? Tatizo hili mara nyingi husababishwa na huambatana na mambo yafuatayo:

  • kula vyakula vyenye mafuta mengi ambayo huchelewesha tumbo kufunguka kwa ajili ya usagaji wa chakula
  • kunywa vinywaji vyenye carbonates, na ulaji wa vyakula vyenye gesi kama maharagwe, kutafuna peremende za gamu, vitunguu, kabichi na kadhalika
  • msongo wa mawazo na hasira
  • kula haraka haraka na kula ukiongea
  • uvutaji wa sigara
  • magonjwa na maambukizi katika mfumo wa chakula hasa kwenye tumbo na utumbo ambayo huzuia kusagwa na kufyonzwa kwa chakula

Jinsi ya kukabiliana na hali hii

Kunywa chai ya tangawizi au karafuu itasaidia kupunguza gesi.

Unaweza kunywa glasi moja ya juisi ya limau baada ya kula.

Tafuna mbegu za maboga kwa sababu zinasaidia kulainisha mfumo wa chakula na umeng’enyaji.

Lalia ubavu na pumua kwa kasi ili kupunguza gesi tumboni.

Kuikunja miguu na uikalie huku ukinyoosha mikono na kuinamia mbele itasaidia.

Kuongeza kasi ya mfumo wa chakula kufanya kazi na kuondoa gesi.

Fanya mazoezi mepesi ya kutembea na kurukaruka.

Kula na tafuna chakula taratibu na epuka vyakula vyenye gesi na mafuta mengi.

Nenda hospitali kama tatizo hili linaambatana na kuharisha, kutapika, maumivu makali ya tumbo, kinyesi chenye rangi tofauti au damu na maumivu ya kifua.

You can share this post!

Jinsi ya kuandaa pilau ya mboga mbalimbali

Pigo kwa Arsenal baada ya kipa Andre Onana kuhiari kutua...