• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
BENSON MATHEKA: Hatua zichukuliwe upesi kukabili matatizo ya akili

BENSON MATHEKA: Hatua zichukuliwe upesi kukabili matatizo ya akili

NA BENSON MATHEKA

IDADI ya raia wanaokumbwa na matatizo ya akili nchini inazidi kuongezeka inavyodhihirishwa na visa vya watu kuua jamaa zao na kujitoa uhai.

Hii ni hali inayosikitisha sana na ni hatari kwa nchi hasa ikizingatiwa kuwa wengi wanaokumbwa na hali hii wana umri mdogo wakiwemo wanafunzi. Visa vimeripotiwa vya wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu kujitoa uhai au kutekeleza mauaji.

Haipiti mwezi mmoja kabla ya kisa kinachohusishwa na matatizo ya akili kuripotiwa miongoni mwa maafisa wa usalama.

Wataalamu wametambua hali ngumu ya uchumi, kupoteza matumaini na matumizi ya dawa za kulevya na ulevi wa kupindukia kama baadhi ya mambo yanayosababisha ongezeko la matatizo ya akili.

Mwaka jana, serikali, kupitia Wizara ya afya ilikiri kwamba athari za janga la corona zimechangia kuongezeka kwa watu walio matatizo ya akili ukiwemo msongo wa mawazo.

Ingawa wizara ilisema imeweka mikakati ya kukabili hali hii, inaonekana huenda haikutekelezwa kikamilifu au haijakuwa na matokeo bora. Kuna haja ya hatua madhubuti kuchukuliwa, tena kwa haraka, kuhakikisha hali hii imekabiliwa ipasavyo kabla ya kubadilika kuwa janga nchini.

Kwa vile, wataalamu wametambua kinachosababisha hali hii, haifai kuchelewa kuchukua hatua kwa kuwa inahatarisha nchi. Ili kuokoa hali, serikali haina budi kuwekeza zaidi katika afya ya akili na kutekeleza kikamilifu sheria zilizopo za kukinga umma kama ya kukabiliana na matumizi ya dawa za kulevya.

Muhimu kabisa ni kuhakikisha maisha ya Wakenya yanaimarika kwa kuboresha uchumi.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Kuwe na mfumo wa kuwekeza zaidi katika elimu ya...

DKT FLO: Nitaongezaje unene kifuani na makalio?

T L