• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
OSMAN MOHAMED: Raia wasiogope kuwasilisha malalamishi kwa afisi za Ombudsman

OSMAN MOHAMED: Raia wasiogope kuwasilisha malalamishi kwa afisi za Ombudsman

Na OSMAN MOHAMED

MNAMO 1971, TUME iliyoundwa kuchunguza mfumo wa Utumishi wa Umma na Mishahara (maarufu kama Tume ya Ndegwa), ilipendekeza kubuniwa kwa kwa ofisi ambapo wananchi wangewasilisha malalamishi yao dhidi ya serikali.

Pendekezo hilo lilitokana na utoaji wa huduma duni katika sekta ya Utumishi wa Umma.

Kulikuwa na kuchelewa kwa huduma katika afisi za serikali, ufisadi, mapendeleo, ubaguzi na watu kunyimwa huduma bila sababu maalumu.

Ofisi ya “ombudsman” (om-budzi-man) “Mwakilishi” iliundwa ili kuwasaidia watu binafsi au makundi ya watu, kutatua malalamishi yao dhidi ya taasisi za serikali.

Pia, huchunguza tabia za watumishi wa umma na kuripoti kwa bunge. Afisi hii pia ina mamlaka ya kuwasilisha malalamishi hayo mahakamani ili walalamishi watendewe haki.

Kwa ufupi, afisi hii ina jukumu la kufuatilia utekelezaji wa Sura ya Nne ya Katiba, ambayo inahusika na haki msingi.

Chini ya Sheria ya mwaka 2011, tuna mamlaka ya kuchunguza; utumizi mbaya wa mamlaka, watu kutoheshimiwa, kunyimwa haki, na ujeuri au ubaguzi wa maafisa wanaoshikilia afisi za umma.

Hueneza uhamasishaji kuhusu sera na kanuni zinazohusiana na jinsi ya kupata haki kati ya mambo mengine.

Chini ya sheria ya Haki ya Kupata Habari (2016), afisi hiyo hufuatilia jinsi umma unavyopata habari muhimu kutoka kwa serikali.Tangu ilipoundwa miaka 10 iliyopita, afisi hii imefungua matawi katika miji ya Mombasa, Eldoret, Kisumu, na Isiolo.

Pia, kuna mipango ya kuanzisha afisi nyingine kwenye miji ya Garissa na Nyanyuki.

Malalamishi mengi yanahusu maafisa wa serikali waliostaafu kucheleweshewa pensheni.

Kuna ucheleweshaji hati miliki za mashamba, na watu kunyimwa habari muhimu wanapozitaka.Tume hii imejitolea kutatua malalamishi haya.

Wananchi wanaweza kuwasiliana nayo kwa kutembelea afisi zake, au mitandaoni.

Wavuti ni: www. ombudsman.go.ke na barua pepe: [email protected].

Bw Osman ni mkurugenzi wa mawasiliano.

You can share this post!

Kananu achukua usukani kama gavana Nairobi

TAHARIRI: Kenya ina kila sababu kujali hali ya majirani

T L