• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
Brazil wakomoa Colombia na kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2022

Brazil wakomoa Colombia na kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2022

Na MASHIRIKA

BRAZIL imekuwa timu ya kwanza kutoka Amerika Kusini kufuzu kwa fainali zijazo za Kombe la Dunia za 2022 nchini Qatar baada ya kusajili ushindi wa 1-0 dhidi ya Colombia katika uwanja wao wa nyumbani.

Lucas Paqueta, 24, alikuwa mfungaji wa bao la pekee na la ushindi katika mchuano huo uliotandaziwa ugani Neo Quimica Arena jijini Sao Paulo. Kiungo huyo wa Olympique Lyon nchini Ufaransa alishirikiana vilivyo na wanasoka wawili wa Paris Saint-Germain (PSG) – Marquinhos na Neymar.

Brazil ambao ni mabingwa mara tano wa Kombe la Dunia wangali na michuano sita zaidi za kusakata katika safari ya mechi za vikosi vya Amerika Kusini kuelekea Qatar. Kufikia sasa, masogora hao wa kocha Adenor ‘Tite’ Bacchi wamepoteza alama mbili pekee kutokana na mechi 12 zilizopita na pengo la pointi tisa linatamalaki kati yao na nambari mbili Argentina.

Mechi ijayo itakayosakatwa na Brazil ni gozi la ugenini litakalowakutanisha na washikilizi wa taji la Copa Amerika, Argentina, katika mji wa San Juan mnamo Novemba 16, 2021.

You can share this post!

Aguero atakuwa radhi kustaafu soka mnamo Februari 2022

Aliyepandishwa kuwa refa wa Ligi ya Kitaifa Daraja ya...

T L