• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 12:11 PM
Crescent United: Timu wembe inayoinua soka mashinani

Crescent United: Timu wembe inayoinua soka mashinani

NA PATRICK KILAVUKA

CRESCENT United inapatikana Mlolongo, kaunti ndogo ya Mavoko, Kaunti ya Machakos.

Inayo matumaini tele kunyakua taji la Ligi ya Mavoko msimu huu.

Ilianzishwa mwaka wa 2014 na wanasoka 13 waliokuwa na umri chini ya miaka chini ya kumi mitano.

Kocha Josephat Osoro ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa shule ya upili ya Upper Hill kabla kusazwa na jeraha, anasema nia yao ilikuwa kukung’uta maovu ya kijamii, utovu wa nidhamu na usalama pamoja na kukuza talanta za mashinani ambazo nimejikuza ndani mwa vipaji vya wanadimba hawa ambao wamekomaa kumenyana katika ligi na kucheza vipute.

Wanaoshirikiana na mkufunzi huyo kuvumisha soka ni meneja wa timu Lameck Omondi na naibu wa kocha Silas Simiyu.

Timu ilianza kucheza ligi ya awamu ya kaunti ndogo ya FKF, Mavoko mwaka wa 2017 ikiazimia kuangazia wanachezaji katika ushindani wa kandanda na kupanua uwezo wa wachezaji kujijua zaidi kisoka.

Msimu uliopita ilitamatisha katika nafasi ya sita, japo msimu huu katika ligi ya Mavoko kufikia sasa inaongoza kwa alama 30 sawa na Dabaki United japo zinatenganishwa na magoli mawili.

Hata hivyo, nafasi ya tatu inashikiliwa na Mass iliojumlisha na pointi 26 kufikia kunakiliwa kwa makala.

Wanajivunia matokeo bora kwa kuwaliza Hera 3-0, Mahalashmi 2-0 na Warriors 3-0 mtawalia.

Kujipiga msasa zaidi, imeshiriki katika kipute cha Wavinya Cup 2022 na kubanduliwa robo fainali ambapo washindi waliibuka kuwa Chelsea.

Kuimarisha nguzo ya safu ya kiungo na fowadi, imesajili kiungo Frank Mwangangi na Mafowadi Noel Ngatha na Moses Yuobi.

Kwa vile ni timu ya kujitegemea, changamoto kuu hutokana na ufadhili wa kuipiga jeki kwani wanahitaji kutembelea sehemu mbalimbali lakini wanabanwa na gharama za ziada kwa sababu ni kujitolea kwa wanasoka hawa pamoja na kushikwa mkono na wadau wa timu, timu inasukuma kuguruduma na kukuza vipawa ambavyo vingine kuwa kiporo.

Kikosi cha Crescent United cha Mlolongo kikicheza mechi ya kujipima nguvu dhidi ya Real Stars United ugani Kihumbuini awali. PICHA | PATRICK KILAVUKA

Kocha Osoro anasema uwiano mwema katika timu na ushirikiano wa sako kwa bako pamoja na kushuariana, timu imekuwa na mnato mithili wa jamii.

Wadau wa timu wanasema wangependa kumpa mkono wa shukran Dan Otieno wa Odibet na MCA wa Mavoko Daniel Ndwike kwa uhisani wao wa sare.

Mipango ya timu ni kushiriki ligi za juu kuweka wanakandanda wao katika ramani ta kitaifa kwani wanaamini mashinani kumeiva soka ila, namna ya kutambuliwa ndiyo finyu.

Mbali na kushiriki ligi za ushindani ikwemo ya Shirikisho la Soka Nchini wachezaji waweza kupata jukwaa.

Kikosi cha Crescent United Mlolongo kikipiga zoezi kabla kurudi uwanjani wakati wa mechi yao ya kujipima nguvu dhidi ya Real Stars United ugani Kihumbuini awali. PICHA | PATRICK KILAVUKA
  • Tags

You can share this post!

PAUKWA: Ama kweli nzi kufa kidondani si haramu

Teknolojia kutawala Jamhuri Dei ya leo Jumatatu

T L