• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 9:50 AM
Erzurumspor anayochezea Omolo yaendelea na ufufuo Ligi Kuu nchini Uturuki

Erzurumspor anayochezea Omolo yaendelea na ufufuo Ligi Kuu nchini Uturuki

Na GEOFFREY ANENE

BB Erzurumspor anayochezea kiungo Johanna Omolo inaelekea kujiondoa katika maeneo hatari ya kutemwa kutoka Ligi Kuu ya Uturuki baada ya kuchapa wenyeji Gaziantep 3-2 Jumapili.

Erzurumspor ilipata ushindi huo wa tatu mfululizo kupitia mabao ya kipindi cha pili yaliyopatikana kutoka kwa Ricardo Gomes dakika ya 54, Hasan Hatipoglu (59) na Rahman Bugra Cagiran (84). Gaziantep ilipata mabao yake kupitia Muhammet Demir dakika ya 69 na 90. Omolo alipumzishwa dakika ya 67.

Erzurumspor sasa inakamata nafasi ya 18 kwa alama 37 kwenye ligi hiyo ya timu 21. Timu nne za mwisho zitatemwa kwa hivyo Erzurumspor kwa sasa bado inahitaji kushinda michuano kadhaa ndiposa ijiondoe katika mduara hatari.

Erzurumspor, ambao waliingia Ligi Kuu baada ya kukamilisha Ligi ya Daraja ya Pili katika nafasi ya pili msimu 2019-2020, wako nyuma ya nambari 16 Kasimpasa na nambari Istanbul Basaksehir kwa tofauti ya ubora wa magoli.

Wataalika Basaksehir (Aprili 29), kuzuru Fenerbahce wanaoshikilia nafasi ya pili (Mei 3), Kasimpasa (Mei 9) halafu wafunge msimu dhidi ya nambari tano Alanyaspor (Mei 12).

  • Tags

You can share this post!

Mwenda asisitiza ligi itakamilika

Klabu ya Masud Juma yaendelea kuzama Ligi Kuu Morocco