• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:55 AM
Kinara wa mashindano ya baiskeli nchini Ujerumani afurushwa Tokyo, Japan kwa sababu ya ubaguzi wa rangi

Kinara wa mashindano ya baiskeli nchini Ujerumani afurushwa Tokyo, Japan kwa sababu ya ubaguzi wa rangi

Na MASHIRIKA

MKURUGENZI wa Shirikisho la Uendeshaji Baiskeli nchini Ujerumani, Patrick Moster amefurushwa kwenye Olimpiki za Tokyo na kuamrishwa kurejea nyumbani kwao baada ya kutoa kauli zilizoashiria ubaguzi wa rangi.

Moster alitoa kauli hizo katika mahojiano aliyofanyiwa na runinga moja kutoka Ujerumani TV baada ya mwendeshaji baiskeli Nikias Arndt wa Ujerumani kuonekana akiwafukuza na kutusi Azzedine Lagab wa Algeria na Amanuel Ghebreigzabhier wa Eritrea kutokana na rangi ya ngozi zao.

Moster alitetea hatua hiyo ya Arndt badala ya kuikashifu kwenye mahojiano yake runingani.

Katika taarifa yao, vinara wa Kamati ya Kitaifa ya Olimpiki nchini Ujerumani walisema, “Moster hataendelea kutekeleza majukumu yake katika kikosi cha Ujerumani kilichoko jijini Tokyo.”

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Rais awaongoza Wakenya kumwomboleza mumewe waziri Amina...

Malalamiko tele chombo cha kukagua mizigo kikiharibika...