• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 7:50 AM
Kipa Mendy aweka rekodi

Kipa Mendy aweka rekodi

NA MASHIRIKA

LONDON, UINGEREZA

GOLIKIPA wa Chelsea Edouard Mendy, Jumanne usiku aliweka historia kwa kuwa kipa wa kwanza kucheza mechi nyingi za Klabu Bingwa bila kufungwa bao.

Baada ya kuichapa Lille 2-0 katika mkondo wa kwanza 16-bora wa michuano hiyo ya bara Ulaya, raia huyo wa Senegal ameenda mechi 14 bila kufungwa kati ya 18 alizocheza.

Mendy amekuwa na msururu mzuri tangu ajiunge na Chelsea mwaka uliopita, huku akijivunia ushindi katika mashindano yote aliyoshiriki.

Mbali na kuisaidia klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Klabu Bingwa barani Ulaya, kadhalika kipa huyo aliisaidia timu yake ya taifa kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) pamoja na ubingwa wa FIFA Club World Cup akiwa na Chelsea majuzi.

Ushindi wa Chelsea dhidi ya Lille ambao ndio mabingwa wa ligi kuu ya Ufaransa umewaweka katika nafasi nzuri ya kuwa na kazi rahisi katika mechi ya marudiano itakayochezwa Machi 16 ugani Stade Pierre-Mauroy.

Chelsea waliingia uwanjani wakijivunia ushindi mara tano mfululizo, ukiwemo mara mbili kule Abu Dhabi wakati wa michuano ya Club World Cup.

Mabingwa hao wa bara Ulaya walifanikiwa kupata bao la kwanza dakika ya nane kupitia kwa Kai Havertz aliyefunga kwa kichwa. Romelu Lukaku aliyetarajiwa kuanza, hakupata nafasi kikosini.

Christian Pulisic aliongeza bao la pili mapema katika kipindi cha pili.

Licha ya ushindi huo muhimu, Chelsea ilipatwa na pigo baada ya kiungo mahiri Mateo Kovacic na mshambuliaji Hakim Ziyech kujeruhiwa na kutolewa katika kipindi cha pili, wakati kikosi hicho kinajiandaa kupambana na Liverpool katika fainali ya Carabao Cup.

You can share this post!

Rais amtaja Raila mrithi wake Ikulu

Fundi ashtakiwa kuiba pikipiki

T L