• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
Koth Biro: Leads yakiri kibarua kigumu robo fainali

Koth Biro: Leads yakiri kibarua kigumu robo fainali

Na JOHN KIMWERE

KOCHA mkuu wa Leads United, Wilston Issa amesema kuwa wanatarajia kibarua kigumu kwenye mechi ya robo fainali kuwania taji la Koth Biro mwaka huu.

Leads United imepangwa kucheza na Ruaraka Allstars iliyomaliza ya pili kwenye ngarambe hiyo muhula uliyopita. ”Ni kweli tumepania kujituma kwa udi na uvumba kwenye mchezo huo lakini tunafahamu bayana kuwa haitakuwa mteremko,” kocha huyo alisema na kuongeza kuwa wanafahamu wapinzani wao wamejipanga kuwalipua.

Leads ambayo hushiriki Ligi ya Taifa Daraja la Pili inajivunia kutawazwa mabingwa wa taji la Tim Wanyonyi Super Cup mara mbili mfululizo.Robo fainali zitaanza Jumatatu ijayo (24.01) huku fainali ikitazamiwa kuchezwa Januari 29.

Kwenye mechi za raundi ya 16 bora Leads ilitolewa kijasho kabla ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Sharps. Timu zingine zitakaoshiriki robo fainali ni:Wenyeji Youth, Mlango Kubwa, Mathare Combined, Team Dandora,

A 1000 Sportive na Borussia FC. Wenyeji Youth ilikomoa kaka zao Wenyeji United 3-2, Borrusia FC ilizaba Biafra Kamaliza 2-0, Mlango Kubwa ilibeba 2-0 dhidi ya Wendani United, A 1000 Sportive ilinyuka Kisima 2-0, Mathare Combined ilipiga Huruma Kona 3-1 nayo Ruaraka Allstars iliadhibu Slumscores 2-1.

Ngarambe ya muhula huu ilishirikisha jumla ya timu 46 kutoka mitaa mbali mbali katika Kaunti ya Narobi. Bingwa wa mwaka huu atapokea kitita cha Sh300, nambari mbili atatuzwa Sh100,000, nambari tatu na nne watatia mfukoni Sh 50,000 na Sh20,000 mtawalia.

You can share this post!

Gael Halima: Chipukizi anayepania kutinga hadhi ya kimataifa

Mahakama yakataa kumpunguzia raia wa Congo dhamana ya...

T L